Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiweka jiwe la msingi katika jengo la kituo cha utoaji wa huduma za UKIMWI linalojengwa kwa lengo la uboreshaji wa vituo 20 vya huduma ya watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI katika kituo cha Afya cha Ipogolo Mkoani Iringa Novemba 22, 2019.wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya hiyo Mhe. Richard Kasesela.
Na.Mwandishi Wetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Afya Ipogolo Manispaa ya Iringa ikiwa ni sehemu ya mradi wa uboreshaji wa vituo 20 vitakavyotoa huduma za UKIMWI kwa wasafirishaji wa masafa marefu.
Hafla hiyo iliyofanyika tarehe 22 Novemba, 2019 katika Kata ya Ruaha Kijiji cha Ipogolo mkaoni Iringa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Dawa za Kulevya ,Omari Badweli (Mb) wa Bahi, Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt Leonard Maboko, Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe, Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Hamad Ahamad Njovu na wawakilishi kutoka , Ofisi ya Rais -TAMISEMI , Wizara Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano , Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ,TANROADS pamoja na watendaji kutoka Halmashauri.
Kabla ya kuweka Jiwe la Msingi, Waziri Mhagama alipongeza juhudi za Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi za uratibu na utekelezaji wa masuala ya mapambano dhidi ya UKIMWI kwa kuhakikisha ujenzi wa vituo 20 unaanza katika maeneo yenye vichocheo vya maambukizi ikiwemo barabara zinazotumiwa na wasafirishaji wa masafa marefu.
“Uboreshaji wa majengo ya Kituo cha Afya cha Ipogolo kwa niaba ya maboresho kama haya kwenye vituo 20 vilivyoko kando kando ya barabara kuu ya Dar es Salaam hadi mipaka ya Kasumulu (Tanzania/Malawi) na Tunduma (Tanzania/Zambia) ili kutoa huduma za udhibiti wa VVU/UKIMWI kwa ufanisi kwa wasafirishaji wa masafa marefu pamoja na jamii zinazoishi kwenye maeneo hayo utasaidia kuendeleza mapambano dhidi ya UKIMWI kwa kuzingatia mchango utakaotokana na ujenzi wa vituo hivi”.
Waziri alieleza, ujenzi huo unaotekelezwa kupitia programu ya sattf barabara kuu ya Dar es salaam hadi mipaka ya Tunduma/Nakonde (Zambia) na Kasumulu/Songwe(Malawi) kwa kutambua umuhimu wa huduma za afya kwa wananchi wa Tanzania na kwa kuzingatia misingi ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) pamoja na marekebisho yake. Uboreshaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi ni moja ya utekelezaji wa haki za binadamu katika kupata huduma za afya na haki ya kuishi.
Aidha alieleza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha wananchi hususani wanaoishi na virusi vya Ukimwi (WAVIU) wanapata haki ya matibabu ya VVU na magonjwa nyemelezi, haki ya kutokubaguliwa na haki za kushirikishwa. WAVIU nao pia wana wajibu wa kulinda wengine wasipate maambukizi ya VVU.
Kwa kuzingatia Sheria ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI (Kuzuia na Kudhibiti) Na. 28 ya mwaka 2008 na Sera ya Taifa ya UKIMWI ya mwaka 2001 zote zinatoa wajibu kwa kila mtu kulinda na kutetea haki za WAVIU.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akizungumza kwa niaba ya Mkoa wa mkoa huo Mhe.Ally Hapi alieleza kuwa, ujenzi wa vituo hivyo utasaidia kupunguza maambukizi na kuongeza tija katika huduma zitakazotolewa kupitia vituo hivyo.
“Ujenzi wa kituo hiki uwe chachu ya kuendelea kutumia huduma za Ukimwi ikiwemo matumizi sahihi ya dawa za kufubaza virusi ili kuendelea kuwa na afya njema na kushiriki vyema katika shughuli za kimaendeleo nchini’”alisema Kasesela
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa NACOPHA, Leticia Kapela alieleza kuwa, jamii haina budi kuendeea kuunga mkono jitihada hizo na kuhakikisha tatizo la unyanyapaa linatokomezwa kabisa na kuendelea kuishi kwa upendo, usawa na amani.
“Uzinduzi wa leo umeonesha upendo na kujali masuala ya watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI hiyo niwaombe viongozi wa dini kuungana na jitihada za mapambano haya kwa kuzitumia nafasi zenu kukemea masuala ya unyanyapaa kwa watu wanaosihi na maambukizi.
“Viongozi wa dini tuendelee kuliangalia hili kwa kukemea masuala ya unyanyapaa kwa malengo ya kuifikia 909090 na ikumbukwe hakuna sababu ya kufanya hivyo kwa kuzingatia usemi usemao asohili analile,”alisisitiza Leticia.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Leonard Maboko mara baada ya kuwasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa alipofika kwa ajili ya zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi katika kituo cha Afya cha Ipogolo kwa ajili ya utoaji huduma za UKIMWI kituoni hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akitoa taarifa hali ya UKIMWI katika mkoa huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Ally Hapi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembea mkoani hapo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisalimia na baadhi ya wagonjwa wanaosubiri kupewa huduma katika kituo cha Afya cha Ipogolo Mkoani Iringa alipotembelea kuweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la kuhudumia watu wanaoishi na VVU.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akimfurahi mtoto aliyezaliwa katika Kituo cha Afya cha Ipogolo na kupewa lake (Jenista) alipotembelea kituo hicho.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akimjulia hali Mzee Marko Mveyange aliyelazwa katika Kituo cha Afya cha Ipogolo kwa ajili ya matibabu.
Msimamizi Mkuu wa huduma za matibabu na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU (CTC) Dkt. Onesmo Ng’ande akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama kuhusu jengo linaloendelea kujengwa kwa ajili ya utoaji wa huduma za UKIMWI alipotembelea na kuweka jiwe la msingi ujenzi huo katika Kituo cha Afya cha Ipogolo Iringa.
Msimamizi Mkuu wa huduma za matibabu na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU (CTC) Dkt. Onesmo Ng’ande akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama kuhusu jengo linaloendelea kujengwa kwa ajili ya utoaji wa huduma za UKIMWI alipotembelea na kuweka jiwe la msingi ujenzi huo katika Kituo cha Afya cha Ipogolo Iringa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akihutubia wananchi wa Ipogolo walioshiriki wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Jengo la Kituo cha utoaji wa huduma za UKIMWI linaloendelea kujengwa katika kituo cha Afya cha Ipogolo mkoani Iringa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko akizungumza wananchi wa Ipogolo (hawapo pichani) walioshiriki wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Jengo la Kituo cha utoaji wa huduma za UKIMWI linaloendelea kujengwa katika kituo cha Afya cha Ipogolo mkoani Iringa.
Baadhi ya washiriki waliohudhurika katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Jengo la Kituo cha Utoaji wa Huduma za UKIMWI lililopo katika Kituo cha Afya cha Ipogolo Iringa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani)
Mwenyekiti wa NACOPHA, Leticia Kapela akitoa salamu wakati wa hafla hiyo.
Mwakilishi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Dawa za Kulevya Mhe.Omari Badwel (Mb) wa Bahi akitoa salamu za kamati hiyo wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasele akitoa salamu za Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo wakati wa hafla hiyo.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment