Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. George Simbachawene (wa pili kushoto) akiwa na wabunge wa
majimbo ya Pemba katika ziara kutembelea miradi ya Mfuko wa Jimbo wilaya za
Wete na Chakechake.
Na.Robert Hokororo. -Pemba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. George Simbachawene amewataka watendaji wa Serikali
wanaosimamia miradi mbalimbali ya maendeleo kuzingatia sheria wanapotekeleza
shughuli zao.
Mhe.Simbachawene ametoa kauli hiyo wilayani Chakechake, Pemba
wakati wa majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya Mfuko wa
Jimbo katika wilaya za Wete na Chakechake kisiwani Pemba.
Alisema kuwa Katika kuhakiksha mfuko unatekelezwa vizuri
watendaji hao wana wajibu wa kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika hatua
zote za utekelezaji wa miradi ili mwishoni waweze kuandika taarifa.
Akizungumza na wabunge wa majimbo yaliyopo katika wilaya
hizo pamoja na watendaji hao alibainisha kuwa nafasi ya mbunge na kamati
inayosimamia mradi kupitia Mfuko wa Jimbo ni kubwa na wanapaswa kufanya kazi
hadi kukamilika kwake.
“Wajibu wa kamati unaendelea hadi mradi ukamilike kwani
baadaye mtatakiwa kuandika ripoti ya nini kimefanyika tangu mwanzo wa mradi
hivyo kukataa kushirikiana na mbunge hakuna tija ni kinyume cha utaratibu na
sheria na pia mbunge anapaswa kusimamia mradi kuona kama kuna value for money,” alisisitiza.
Awali wakitoa maoni yao kwa waziri baadhi ya wabunge akiwemo
Maida Hamed Abdallah wa Viti Maalumu Mkoa wa Kaskazini Pemba waliomba wawe wanashirikishwa
katika kamati za miradi ndani ya majimbo pamoja na kuwa wao hawana mufuko wa
jimbo.
Walisema kuwa kutokana na wao kutokuwa sehemu ya kamati
inakuwa ni jambo gumu kuweza kulitolea ufafanuzi wa namna gani fedha za mfuko
zimetumika kwakuwa wanakosa taarifa muhimu.
Miradi aliyotembelea Simbachawene ni mradi wa skuli ya
maandalizi Kangagani na mradi wa maji safi na salama Wingwi Mjazana iliyopo
Wilaya Wete. Pia alitembelea miradi skuli ya Vikungani na mradi wa umeme wa
Pujini iliyopo Wilaya ya Chakechake.,
Waziri Simbachawene katika ziara hiyo pia alitembelea
Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Tunguu, Unguja ambapo alipata nafasi ya
kukutana na baadhi ya watumishi na kusalimiana nao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. George Simbachawene akiwa katika skuli ya maandalizi ya
Kangagani wakati wilayani Wete, Pemba wa ziara ya kutembelea miradi ya Mfuko wa
Jimbo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
Mhe. George Simbachawene akifurahia jambo na wabunge alioambatana nao kwenye
ziara ya kukagua miradi ya Mfuko wa Jimbo wilaya za Wete na Chakechake mara
baada ya kuwasili Ofisi za Makamu wa Pili wa Rais Pemba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho
ya ziara wilayani Chakechake. Kulia kwake ni Mbunge wa Mtambile, Mhe. Masoud
Abdallah Salim.
Wabunge wa majimbo ya Pemba wakiwa katika kikao cha
majumjisho ya ziara ya kukagua miradi ya Mfuko wa Jimbo katika wilaya za Wete
na Chakechake.
Wataalamu kutoka halmashauri za wilaya na mabaraza ya
miji wakiwa katika kikao cha majumjisho ya ziara ya kukagua miradi ya Mfuko wa
Jimbo katika wilaya za Wete na Chakechake.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. George Simbachawene (katikati)n akiendesha kikao cha majumuisho
ya ziara ya kukagua miradi ya Mfuko wa Jimbo wilaya za Wete na Chakechake.
Kushoto ni Mbunge wa Mtambile, Mhe. Masoud Abdallah Salim na kulia ni Kaimu
Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Lupi Mwaikambo.
Kaimu Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Lupi
Mwaikambo akifafanua jambo katika kikao cha majumjuisho ya ziara ya kukagua
miradi ya Mfuko wa Jimbo wilaya za Wete na Chakechake, Pemba.
No comments:
Post a Comment