Habari za Punde

Serikali Iwametaka Kuingiza Masuala Mtambuka Kwa Watu Wenye Ulemavu.

Na.Takdir .Suweid . Maelezo Zanzibar.
Maafisa waratibu wa masuala ya Watu wenye ulemavu Wizara za Serikali wametakiwa kuyaingiza masuala mtambuka ikiwemo ya Watu wenye ulemavu ili kuweza kuleta mabadiliko katika Taasisi zao na Taifa kwa ujumla.

Hayo yameelezwa na Afisa Tathmini na Ufuatiliaji kutoka Wizara ya Watu wenye ulemavu Zanzibar Khamis Machano Kheir wakati alipokuwa katika kikao cha robo ya pili ya utendaji,kikao ambacho kimefanyika Wizara ya Afya Zanzibar.

Amesema Wizara za Serikali zimeweka Dira,Malengo na Dhamira hivyo iwapo watayaingiza masuala hayo katika Wizara zao itaweza kupunguza Migogoro na ndoa za kiholela.

Amefahamisha kuwa masuala Mtambuka ni muhimu kwa sababu yanasaidia kupata taarifa kiurahisi na kuzingatia masuala ya kiutendaji.

Hata hivyo amesema iwapo masuala ya Watu wenye ulemavu hayatoingizwa katika mipango yao,yanaweza kusababisha athari ya kupunguza uzalishaji wa nguvu kazi za Taifa,kuwepo kwa hali tegemezi katika jamii,kuongeza makundi hatarishi na kuibua migogoro ndani ya familia inayopelekea Talaka na kutengana.

Kwa upande wake Afisa mratibu wa masuala ya Watu wenye ulemavu kutoka Wizara ya elimu na mafunzo ya elimu Zanzibar Mohammed Mwinyi Ramadhani amesema Wizara hiyo imeweka utaratibu wa kuwafundisha Waalimu mbinu za kuweza kuwabaini Wanafunzi wenye mahitaji maalum ikiwemo wenye ulemavu ili waweze kuwasomesha kwa ufanisi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.