Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano wa
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Josephat Kagirwa akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo
pichani), kuhusu Fursa za Mkutano wa Wafanyabiashara wazawa wa Tanzania wanasafirisha
bidhaa kwenda India ambao ATCL imeandaa jukwaa hilo ili kuimarisha biashara kwa
kutumia ndege za ATCL zinazofanya safari zake kutoka Dar es Salaam-TANZANIA
kwenda Mumbai-INDIA.
Na.Mwandishi Wetu-MAELEZO.
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), limeandaa safari kwa
wafanyabiashara wazawa itakayofanyika Machi 4, 2020 kwenda Mumbai India
kwaajili ya kukuza biashara baina ya nchi Tanzania na nchi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es
Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano wa ATCL, Josephat Kagwirwa
alisema kuwa safari hiyo itahusisha wafanyabiashara na abiria wa kawaida na
lengo la safari hiyo maalum ni kukuza biashara kwa wafanyabiashara wa Tanzania kwa
kuwaunganisha na soko la India.
“Katika mkakati wa Biashara wa ATCL ambao ulianza 2017
ambao utamalizika 2022, tumeandaa safari maalum kwa wafanyabiashara wazawa
nchini kwenda India kwa jukwaa la kibiashara la siku mbili kuanzaia Machi 5
hadi machi 6,2020, fursa ambayo itawasaidia wafanyabiashara kupata fursa masoko
kwani watatembelea maeneo mbalimbali ya biashara ikiwemo kituo maalum ambapo
bidhaa zote duniani hufikia na kusambazwa”, alisema Kagirwa.
Kagirwa alisema kuwa tiketi zitapatikana kwa dola za
kimarekani 500 ambayo itahusisha kusafiri kwenda Mumbai na kurudi Dar es Salaam
pamoja na huduma za kutembelea masoko mbalimbali na dola 700 kwenda na kurudi,
huduma za kutembelea masoko pamoja na malazi.
ATCL imekuwa mdau mkubwa wa wafanyabiashara katika
masoko ya nje kwani mpaka sasa imefanya safari za kwenda nje takribani mara saba
ambazo zimekuwa na tija kubwa.
Serikali ya Awamu ya Tano hadi sasa imenunua ndege
nane kwaajili ya kulifufua shirika la ndege la ATCL na matunda yake yanaanza
kuonekana na miongoni mwake ni hili la wafanya biashara wa Tanzania kuanza
kufaidi uwekezaji huo mkubwa.
No comments:
Post a Comment