Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein Ajumuika na Wananchi Katika Maziko ya Marehemu Ali Salim Hafidh Aliyekuwa Msaidi wa Rais Hutuba.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein , akijumuika na Waumini  wa Dini ya Kiislam katika Sala ya kuuombea Mwili wa Marehemu Ali Salim Hafidh, aliyekuwa Msaidizi wa Rais Hutuba , Sala hiyo imefanyika katika Masjid Jamiu Zinjbar Mazizini(kushoto  kwa Rais) Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe.Dkt. Amani Karume na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi 

Rais wa Zanzibaer na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Waumini wa Dini ya Kiislam wakiitikia dua ikisomwa na Sheikh.Muhiddin Ahmad (Maalim Siasa) baada ya Sala ya kuusalia mwili wa Marehemu Ali Salim Hafidh aliyekuwa Msaidizi wa Rais Hutuba. iliofanyika katika Masjid Jamiu Zinjbar Mazizi Unguja leo.14-2-2020.RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Ali Salim Hafidh, aliyekuwa Msaidi wa Rais Hutuba , maziko hayo yamefanyika katika makaburi ya family Fuoni Mambosasa  Wilaya ya Magharibi “B” Unguja
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein , (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na (kulia kwa Rais) Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe.Dkt. Amani Karume, wakiitikia dua ya kuuombea Mwili wa Marehemu Ali Salim Hafidh, aliyekuwa Msaidi wa Rais hutuba

Wananchi na Ndugu na Jamaa wa marehemu wakiitikia dua ya kumuombea wakati wa hafla ya maziko hayo yaliofanyika katika makaburi ya familia Fuoni Mambosasa Wilaya ya Magharibi "B" Unguja leo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akitowa mkono wa pole kwa Wanafamilia ya Marehemu Ali Salim Hafidh, aliyekuwa Msaidizi wa Rais hutuba, yaliofanyika katika makaburi ya familia Fuoni Mambosasa Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.