Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS AKABIDHI AHADI YA MABATI ZAHANATI YA MPUGUZI SINGIDA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo Febuari 25,2020 amekamilisha ahadi yake aliyoitoa kwa Wananchi wa Kijiji cha Mpugizi kata ya Mwaru Mkoani Singida kwa kumkabidhi fedha Taslim Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe. Elibariki Immanuel Kingu kwa ajili ya kununulia Mabati Mia mbili ya kuezekea Zahanati ya Kijiji hicho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe. Elibariki Immanuel Kingu, baada ya kumaliza mazungumzo kumkabidhi msaada wa fedha kwa ajili ya kununulia Mabati Mia mbili ya kuezekea Zahanati ya Kijiji hicho.
(picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.