Habari za Punde

Mashindano ya kuibua Vipaji vya kuigiza kwa Skuli za Msingi Mwaka 2020

Naibu Waziri wa Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Lulu Msham Abdalla akimkabidhi Cheti cha Ushiriki wa Mashindano ya kuibua Vipaji  vya kuigiza kwa Skuli za Msingi Mwaka 2020 Mwanafunzi Hussein Abdallah kutoka Skuli ya Mtoni Mkoa wa Mjini, hafla iliyofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo.  
Naibu Katibu Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Amour  Hamil  Bakari akizungumza kuhusu kuendeleza utamaduni katika  Mashindano ya kuibua Vipaji  vya kuigiza kwa Skuli za Msingi Mwaka 2020 huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Unguja.
Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa Zanzibar Maryam Hamdani akielezea kufurahishwa kwa Maigizo yaliyoigizwa huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo katika hafla ya Mashindano ya kuibua Vipaji  vya kuigiza kwa Skuli za Msingi Mwaka 2020 .
Mwanafunzi kutoka Skuli ya Konde Ali Seif Masoud akichora Picha   katika  Mashindano ya kuibua Vipaji  vya kuigiza kwa Skuli za Msingi Mwaka 2020 huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Unguja. 
Baadhi ya Waalikwa waliohudhuria katika hafla ya Mashindano ya kuibua Vipaji  vya kuigiza kwa Skuli za Msingi Mwaka 2020 huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo .
Baadhi ya Waalikwa waliohudhuria katika hafla ya Mashindano ya kuibua Vipaji  vya kuigiza kwa Skuli za Msingi Mwaka 2020 huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo .
Picha Na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.
Na Rahma Khamis Maelezo                                29/2/2020
Sekta ya sanaa ina mchango mkubwa wa kutoa ajira na kuendeleza vipaji katika jamii kwani inakuza pato la Taifa Nchini.
 Naibu Waziri wa Vijana, Utamadun,i Sanaa na Michezo Lulu Msham Abdallah ameyasema hayo huko Rahaleo katika Ukumbi wa Sanaa wakati akikabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya uibuaji wa vipaji  vya maigizo  na Uchoraji kwa Skuli za Msingi za Serekali.
Amesema adhma ya Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuendeleza kazi za Sanaa na michezo kwani inaimarisha kazi hiyo na kuibua vipaji mbalimbali kwa wanafunzi.
Amesema kuwa Serekali ina vipaji vingi hivyo wamewataka wenye vipaji vya Sanaa yeyote kufika katika Baraza la Sanaa na Michezo kwa ajili ya kujisajili ili kukuza vipaji walivyonavyo.
Aidha Naibu Waziri amezipongeza Wizara zinazoshirikiana kwa kuendeleza michezo sambamba na kuwataka wananchi kufuata sheria na utaratibu katika utendaji wa wa Sanaa zao.
Nae Naibu Ktibu Wizara ya Vijana Sanaa na Michecho Amour Hamil Bakari amesema kuwa ipo haja ya kuongeza Sanaa nyengine ili lengo kazi za Sanaa lifanikiwe kwa wanafunzi.
Aidha amefahamisha kuwa ni jukumu lao kuinua na kuendeleza vipaji kwa wanafunzi hivyo waandaliwe watoto kimichezo wakiwa wadogo ili wachipukie katika Sanaa hiyo.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Michezo Wizara ya Elimu Hassan Tawakal Hairallaw amesema kuwa Wiara imejipanga katika kuendeleza Sanaa nyengine ikiwemo ngonjera na utenzi ili kupata wanafunzi wenye vipaji zaidi
Aidha amesema kuwa michezo ikisimama imara italeta manufaa katika jamii na wala haina athari hivyo wazazi waashauri watoto wao kushiriki katika michezo mbalimbali.
 Washiriki wa mashindano ya uibuwaji wa vipaji vya maigizo wameshiriki kutoka  Skuli ya Fujoni Wilaya ya Kaskazini       Unguja na Skuli ya Ngwachani Wilya ya Kusini Pemba ambapo Skuli ya Fujoni wameshinda na kupata zawadi ya sh, laki tano taslim na cheti cha kushiriki mashindano hayo.
Hata hivyo kwa upande wa washiriki wa Uchoraji ni mwanafunzi Ali Seif Masoud miaka 13 wa darasa la tano kutoka Skuli ya Konde Pemba na mwanafunzi Hussein Abdallah miaka 14 darasa la sita kutoka Skuli ya Mtoni Unguja ambapo mwanafuzi Hussein ndie mshindi katika mashindano ya kuchora na amepata zawadi ya ash, laki mbili taslim na cheti cha ushiriki wa mashindano hayo. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.