Habari za Punde

Mkutano wa Sekta Binafsi Kusikiliza Fursa za Uwekezaji na Changamoto za Wafanyabiashara Kuzipatia Ufumbuzi

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Tellack akieleza kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo katika mkoa wake wakati wa Mkutano wa mashauriano kati ya Serikali na Sekta binafsi ili kusikiliza changamoto za wawekezaji na wafanyabiashara na kuzipatia ufumbuzi uliofanyika katika Manispaa ya Shinyanga
Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu akijibu hoja wakati Mkutano wa mashauriano kati ya Serikali na Sekta binafsi ili kusikiliza changamoto za wawekezaji na wafanyabiashara na kuzipatia ufumbuzi uliofanyika katika Manispaa ya Shinyanga  mkoani Shinyanga.
Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akijibu hoja za masuala ya wafugaji na wavuvi wakati wa mkutano huo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akijibu hoja za masuala ya wafugaji na wavuvi wakati wa mkutano huo.
Mmoja wa wachimbaji wadogo mkoa wa Shinyanga Bw. Ludaki Shaban akiwasilisha kero za ukosefu wa umeme katika maeneo ya uchimbaji wakati wa mkutano wa kusikiliza changamoto za wawekezaji na wafanyabiashara katika mkoa huo.
Mmoja wa wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga Bw. Idsam Mapande akiwasilisha hoja zinazohusu kero za madereva pikipiki wakati wa mkutano huo.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa mkutano huo
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa mashauriano kati ya Serikali na Sekta binafsi ili kusikiliza changamoto za wawekezaji na wafanyabiashara na kuzipatia ufumbuzi uliofanyika katika Manispaa ya Shinyanga wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (hayupo pichani) Februari 26, 2020.
 (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.