Habari za Punde

RPC KILIMANJARO NA RIO KILIMANJARO WAKIANGALIA GARI LILILOTUMIWA NA HAYATI JULIUS KAMBARAGE NYERERE KUTAFUTA UHURU WA TANGANYIKA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi Salum Hamduni, akisoma taarifa fupi iliyobandikwa ndani ya gari lililotumiwa na Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere wakati wa harakati za kutafuta Uhuru wa Tanganyika,kulia ni  Mkuu wa Uhamiaji, Mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Mwandamizi Tunu Ng’ondya, gari hilo limepaki Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi, mkoani Kilimanjaro
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi  Salum Hamduni, akiangalia mandhari ya ndani ya gari lililotumiwa na Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere wakati wa harakati za kutafuta Uhuru wa Tanganyika, gari hilo limepaki Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi, mkoani Kilimanjaro
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi  Salum Hamduni, akimuonyesha Mkuu wa Uhamiaji, Mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Mwandamizi Tunu Ng’ondya  mandhari ya ndani ya gari lililotumiwa na Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere wakati wa harakati za kutafuta Uhuru  wa Tanganyika, gari hilo limepaki Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi, mkoani Kilimanjaro. 
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.