Habari za Punde

Breaking News. Innaa Lillaahi Wainnaa ilayhi Raajiuun: Marin Hassan Marin Amefariki Dunia Leo Jijini Dar es Salaam


Mwandishi wa Habari wa TBC Marini Hassan Marini amefaiki dunia asubuhi ya leo Jijini Dar es Salaam kwa mujibu wa Taarifa ya TBC iliyotolewa hivu punde, kupitia TBC Tv.

Marehemu Marini kabla ya kujiunga na TBC alikuwa akifanya kazi TVZ enzi hizo na Sasa ni ZBC , kabla ya kuhamia TVT kwa sasa ni TBC.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania.(TBC) Dkt. Ayub Rioba anatangaza Kifo Mfanyakazi wa TBC Ndg. Marin Hassan Marin kilichotokea leo asubuhi katika Hospital ya Lugalo Jijini Da es Salaam.

Taarifa zaidi juu ya Kifo cha Marehemu Marin zitaendelea kutolewa na Uongozi wa TBC.

Innaa Lillaahi Wainnaa ilayhi Raajiuun:

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.