Habari za Punde

SMZ Yatangaza Neema Kwa Wakulima wa Mwani Zanzibar.

Wakulima wa Mwani katika Kijiji cha Kibigija Jambiani  wanaojishughulisha na kilimo cha mwani wakiwa katika  eneo lao la kilimo hicho katika bahari ya jambiani wakipanda mwani kama walivyokutwa na mpiga picha wetu wakiwa katika harakati hizo.Na.Himid Choko. Zanzibar.                                                                                           
Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi Amina Salum Ali amesema , Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kuweka  mipango madhubuti, ili kukifanya kilimo cha mwani kuwa  na  manufaa zaidi kwa wakulima na taifa kwa jumla.
Amesema miongoni mwa mikakati inayochukuliwa nI pamoja na kuwapatia wakulima wa zao hilo wataalamu wa kisasa ambao wanaendelea kuwapatia mafunzo na utaalamu  wakulima wa mwani hapa nchini.
Amesema kutokana na taaluma nzuri wanayopatiwa wakulima hao , hivi sasa wamekuwa wakivuna zaidi ya kilo tatu  kwa mbegu moja  ukilinganisha na hapo awali.
Balozi Amina amesema hayo leo wakati  akitowa ufafanuzi wa hoja mbai mbali za wajumbe wa baraza la Wawakilishi kuhusiana na utekelezaji wa Maagizo ya Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi ya Mwaka 2019/2020 kwa  Wizara ya  Biashara na Viwanda.
 Mheshhimiwa  Balozi Amina amelieleza Baraza la Wawakilishi kua, faida nyengine ya elimu ya ukulima wa mwani  ni kuongeza  ubora wa zao hilo na hivyo kusababisha kupanda kwa bei ya mwani kutoka shilingi 400 hadi shilingi 1,800 kwa kilo hivi sasa.
Amesema katika hatua nyenginige Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kujenga kiwanda cha Usarifu wa mwani huko Chamanangwe Pemba ndani ya Awamu hii ili kuongeza soko na thamani ya zao hilo.
Imetolewa na Divisheni ya Itifaki na Uhusiano,                                                           
Baraza la Wawakilishi, Zanzibar.
Jumatatu, Aprili 14, 2020

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.