Habari za Punde

Wazazi na Walezi Kupiga Vita Mimba za Utotoni Kwa Wanafunzi Skuli.

Na. Mwanajuma  Juma.
MWALIMU Mkuu wa skuli ya sekondari ya Paje wilaya ya Kusini Unguja, Ndg.Abdalla Issa Makame amesema kuwa wanahitaji nguvu za pamoja Kati ya wazazi na walezi ili kupiga Vita mimba za utotoni kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Akizungumza na ZBC mwalimu Mkuu huyo amesema kuwa wamekuwa na bidii kubwa ya kuwaelimisha watoto hao pamoja na kuwakataza kufanya vitendo viovu lakini wanavunjika moyo kutokana na baadhi ya wazee na walezi kutowapa ushirikiano.

Amesema kuwa katika miaka ya hivi karibuni kulijitokeza matukio matatu ya wanafunzi kupata ujauzito ambapo kama waalimu wameyachukulia ni mengi na kuongeza kampeni ya kutoa elimu kwa wanafunzi hao.

Hata hivyo amesema kuwa wamekuwa na utaratibu wa kuwapa ushauri nasaha wanafunzi hao kwa kuwaletea watoa nasaha wa nje ili kuwafunza juu ya kujikinga na vitendo viovu ikiwemo kufanya ngono wenyewe kwa wenyewe ha hata kwa watu wa nje.

Amesema kuwa  juhudi hizo zinaonekana kuwa si lolote wala chochote na wanapoona Kuna watoto wamekuwa watukutu zaidi huwaita wazee wao lakini majibu wanayoyatoa yanawavunja moyo.

Hivyo amewataka wazazi na walezi kujitahidi kuwalea watoto wao katika misingi iliyobora na waelewe kuwa wanajukumu la kuwafatilia nyendo zao zote na sio kusaema kuwa wameshindwa.

Jumla ya kesi nne za mimba kwa wanafunzi zimetokea skulini hapo kutoka mwaka 2017 hadi 2020 ambapo mmoja alipata mwaka 2007, wawili walipata mwaka 2019 na tayari wameshajifunguwa na kutarajia kurejea tena skuli huku mmoja akiwa amepata mwaka huu ambae bado anaendelea kwenda shule Kama kawaida

Amesema kuwa katika mimba hizo kesi tatu wanafunzi hao wamepata kutoka kwa wanaume wa nje na kesi moja ni mwanafunzi kwa mwanafunzi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.