Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya
Bw.Richard Mganga.
NA shamimu Nyaki
–WHUSM
Chuo cha Maendeleo ya
Michezo Malya kimefanikiwa kuzalisha wataalam wa kufundisha na kuratibu michezo
mbalimbali nchini ikwemo mashindano ya UMISETA na UMITASHUMTA.
Hayo yamesemwa na
Mkuu wa Chuo hicho Bw.Richard Mganga katika mahojiano maalum ambapo ameeleza
kuwa watalaam waliozalishwa wametokana na kozi zitolewazo chuoni hapo ambazo ni
pamoja na; Michezo kwa ngazi ya Astashahada (Diploma) katika fani ya ualimu wa Michezo
(Coaching),Uongozi wa Michezo (Sports Administration) pamoja na Usimamizi wa
Michezo (Sports Management) lengo ikiwa ni kuandaa watalam wazuri wa kukuza na
kuendeleza michezo nchini.
“Chuo hiki kina utaratibu wa kutoa mafunzo nje
ya chuo pamoja na jamiii inayozunguka chuo hichi ambapo tangu kimeanzishwa
kimekua na utaratibu wa kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa halmashauri mbalimbali
nchini na mwamko umekua mkubwa wa wadau kujifunza michezo”alisema Bw.Mganga.
Aliongeza kuwa Chuo
hicho ndicho pekee kinachotoa kozi za michezo hapa nchini kikilenga kukuza
sekta hiyo kwa kuzalisha wataalamu wenye sifa na viwango vya kimataifa.
Bw.Mganga amezitaja
Halmashauri ambazo zimenufaika na Chuo hicho kupitia mafunzo yaliyotolewa kuwa ni pamoja na
Halmashauri ya Wanging’ombe ya Mkoa wa Njombe,Kalambo Mkoani Rukwa,Iramba ya
Mkoani Singida,Iringa Mjini pamoja na Mpwapwa ya Mkoani Dodoma.
Kwa upande wake,
Mwalimu wa Chuo Hicho Bw.Mohamed Mwiduchi amesema kuwa, Chuo hicho kina viwanja
vizuri ambavyo jamii inayozunguka imekua na utaratibu wa kutumia katika michezo,
huku akieleza kuwa timu ambazo zimekua zikitumia waalimu wa chuo hicho zimekua
zikifanya vizuri katika mashindano mbalimbali.
Bw.Mwiduchi ameongeza
kuwa Chuo hicho kinafundisha michezo ya Mpira wa Pete,Mpira wa Mikono, Mpira wa
Kikapu na Mpira wa Wavu.
Chuo cha Maendeleo ya
Michezo Malya kipo katika Wilaya ya Kwimba Jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment