Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
akizungumza leo Jijini Dodoma na
Waandishi wa Habari kuhusu mfumo
utakaotumika katika michezo ya ligi inayotarajiwa kuanza June mosi, 2020 ambapo ameeleza Michezo
hiyo ni Ligi Kuu, ligi daraja la kwanza, daraja la pili na na kombe la shirikisho la Azam
huku akieleza viwanja vitakavyumika kuwa ni vya Jijini Dar es Salaam na Mwanza.
Na
Eleuteri Mangi-WHUSM, Dodoma.
Serikali
imeruhusu ligi kuu nne kuanza kuchezwa nchini kuanzia Juni 1, 2020 kwa tahadhari
zote ili kumpata bingwa wa ligi hizo na timu mwakilishi katika Kombe la Shirikisho
Barani Afrika.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison
Mwakyembe katika mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dodoma kuhusu uamuzi
wa Serikali wa kuanza kwa ligi hizo baada ya kusitishwa kwa muda kufuatia ugonjwa
mlipuko waugonjwa wa homa kali ya mapafu
(COVID-19) unaosababishwa na virusi vya Corona.
“Tunaruhusu
ligi nne tu kwa kuanzia hali ikiendelea vizuri tunafungulia michezo yote, kwasasa tunafungulia
ligi kuu, ligi daraja la kwanza, ligi daraja la pili na kombe la shirikisho la Azam”
amesema Dkt. Mwakyembe.
Ili
ligi hizo ziweze kuchezwa kwa ufanisi, Dkt Mwakyembe amesema zitachezwa katika
vituo vikuu viwili ambavyo ni Dar es salaa na Mwanza ambapo kwa upande wa kituo
cha Dar es Salaam uwanja vya Taifa, Uhuru na Chamazi na kituo cha Mwanza
viwanja vitakavyotumika ni CCM Kirumba na Nyamagana.
Waziri
Dkt. Mwakyembe amesema kituo cha Dar es Salaam kitahusisha mechi za ligi kuu
pamoja na kombe la shirikisho la Azam
wakati kituo cha Mwanza kitahusisha ligi daraja la kwanza na ligi daraja
la pili.
Dkt.
Mwakyembe ameongeza kuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Hassan Abassi kuanzia
jana ameruhusu wachezaji wa vilabu hivyo waanze kufanya mazoezi ili kujiandaa
na michezo hiyo kwa kuwa wamekaa muda mrefu tangu michezo kusitishwa mapema
mwezi Machi 2020.
Aidha,
Dkt. Mwakyembe amezihimiza taasisi zinazohusika na utaalamu zihakikishe ratiba
ya michezo hiyo inatolewa mapema ili ili mashindano hayo yafanyike kwa ufanisi.
Taasisi
zinazosimamia mashindano hayo ni Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Bodi ya
ligi, Baraza la michezo la Taifa (BMT), Kurugenzi ya Maendeleo ya Michezo
pamoja na wasimamizi wa viwanja.
Vile
vile Waziri huyo ameongeza kuwa Serikali imeweka utaratibu ambao unazidi
kuboreshwa ambapo wachezaji wote watapimwa
joto, na kutahadharisha upimaji huo usiwe na vitu vya kuhujumu timu na
wachezaji hivyo ameiagiza BMT kushirikiana na Wataalam wa Afya katika zoezi
hilo.
No comments:
Post a Comment