Habari za Punde

SERIKALI KUWEKA UTARATIBU UTAKAOWEZESHA TAASISI ZA UMMA NA WATU BINAFSI KUACHA KUAGIZA KADI ZA KIELETRONIKI NJE YA NCHI

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati alipotembelea Kiwanda cha Kuzalisha Vocha na Kadi mbalimbali kilichopo cha Rushabh Investment Limited cha Jijini Tanga wakati wa ziara yake kuona namna wanavyoendelea na uzalishaji kulia ni Mwekezaji wa Kiwanda hicho Rashid Liemba


Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto akikagua kadi mbalimbali  ikiwemo za Kadi za Mpiga kura,Benki na Kadi za NHIF na vyenginezo zilizokuwa zikitoka kwenye mashine za kutengenezea kwenye kiwanda cha Rushabh Investment Limited wakati wa ziara yake leo kulia ni Mwekezaji wa kiwanda hicho Rashid Hamud (Liemba) katikati ni Afisa Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga Gipson George

Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto akikagua kadi mbalimbali  ikiwemo za Kadi Mpiga kura,Benki na Kadi za NHIF na vyenginezo zilizokuwa zikitoka kwenye mashine za kutengenezea kwenye kiwanda cha Rushabh Investment Limited wakati wa ziara yake leo kulia ni Mwekezaji wa kiwanda hicho Rashid Hamud (Liemba)

 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akiangalia mashine mbalimbali kwenye kiwanda hicho kushoto ni Mwekezaji wa kiwanda hicho Rashid Hamud (Liemba) na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji

 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akisisitiza jambo kwa Mwekezaji wa Kiwanda hicho Rashid Hamud (Liemba) kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akisisitiza jambo wakati alipotembelea eneo la Kange ambako kutajengwa kitega uchumi cha Biashara kwa Jiji la Tanga wakati wa ziara yake kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji na kulia ni Afisa Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga Gipson George

Assenga Oscar


Na.Assenga Oscar  -Tanga.

SERIKALI imetakiwa kuweka utaratibu utakaowezesha taasisi za Umma na watu binafsi kuacha kuagiza kadi za kielektroniki nje ya nchi na badala yake watumie zinazozalishwa  nchini ili kujenga uchumi wa viwanda.



Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella alisema hayo leo  wakati alipotembea kiwanda kipya cha kuzalisha vocha na kadi mbalimbali kinachojulikana kwa jina Rushabh Investment Ltd kilichopo Jijini Tanga.



Alisema akiwa kiongozi wa mkoa huo atashawishi Serikali kuweka utaratibu wa bidhaa hizo za Kieletroniki zitakazozalishwa kiwandani hapo zitumike katika sekta mbalimbali hapa nchini.



Shigella alionekana kufurahishwa na uwepo wa kiwanda hicho zaidi baada ya kuelezwa kwamba kiwanda hicho pindi kitakapoanza kazi rasmi, kitakuwa cha pili barani Afrika. Kiwanda kingine kama hicho kipo Afrika Kusini.



"Niombe kwa serikali mara baada ya kiwanda hiki kuanza uzalishaji basi tuachane na uagizaji wa kadi kutoka nje ya nchini kwani sasa huduma hiyo ipo humu nchini, na kwamba itasaidia kujenga uchumi wa nchi, " alisema Shigella.



Mwekezaji wa kiwanda hicho cha Rushabh Investment ltd Rashid Ahmed 'maarufu kwa jina la Liemba' alisema uwepo wa kiwanda hicho licha ya kutoa ajira kwa vijana hapa nchini lakini pia kitakuwa ni ukomboozi kwa nchi za Afrika.



Alisema kuna uhitaji mkubwa wa bidhaa za kadi hasa katika nchi za Afrika kutokana na kukua kwa teklonojia lakini pia nchi nyingi zinalazimika kuagiza na kutengeneza bidhaa hizo nje ya nchi.



Hata hivyo, Liemba ambaye ana kiwanda kingine cha kuzalisha Chokaa ya kisasa kabisa cha Nelkant, alisema  awali walikuwa wakizalisha kadi za simu pekee lakini sasa wamekiongezea uwezo zaidi. 



Alisema wamekiendeleza ili kiweze kuzalisha kadi zote za Kieletroniki zikiwemo kadi za benki, Bima ya afya, kadi ya mpiga kura na kadi nyingine zote, lakini hakijaanza kazi baada ya wataalamu wake watakaoendelea na ufungaji wa mashine kukwama nchini Ujerumani kutokana na ugonjwa wa Covid-19. 



"Kiwanda hiki kilikuwa kianze kazi kabla ya mwezi wa nne lakini wataalamu wa mitambo wako Ujerumanj hivyo wameshindwa kuja kufunga mitambo kutokana na ugonjwa wa Corona.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.