Habari za Punde

Breeking News Kada wa 24 wa Chama Cha Mapinduzi Mhe.Hashim Salum Ajitokeza Kinyanganyiro ya Kuwania Urais wa Zanzibar

Mtangaza Nia Kada wa CCM Mhe. Hashim Salum Hashim mchezaji wa zamani wa Timu ya Miembeni na Timu ya Taifa ya Zanzibar , ajitokeza mchana huu kuchukua Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar 
Akiwa Mwanacha wa 24 kuchukua Fomu ya Urais kupitia CCM 
Kada wa Chama cha Mapinduzi Mhe.Hashim Salum Hashim akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza zoezi la uchukuaji wa fomu ya Urais wa Zanzibar, hafla hiyo imefanyika Afisi Kuu ya CCM Kiswadui Jjini Zanzibar.

MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Hashim Salum Hashim amekuwa Kada wa 24 kuchukua fomu ya kupata ridhaa ya chama  chake ya kuwa Rais wa Zanzibar.

Hashim Salum Hashim aliwasili majira ya saa Sita mchana na kisha kuchukua fomu hiyo na baadae alioata kuongea na waandishi wa Habari.

Akizungumza alisema:

"Nimekuwa Mwana CCM kwa muda mrefu na kwa miaka 15 nimeweza kuwa katika nyadhifa za kichama hadi sasa ikiwemo Mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi.

Pia nafasi ya Katibu Mwenezi Wadi ya Kisima majongoo na Katibu uchumi na fedha tawi la Kikwajuni na zingine mbalimbali." Alisema

Aidha, amesema amesukumwa kuchukua fomu  kwa sababu nia anayo na nguvu anayo hivyo atanataka kuendeleza pale alipoishia Dkt. Ali Mohammed Shein.

"Ninataka kuhakikisha nafikia malengo katika  sekta ya Afya, Jamii na kiuchumi.

Dkt. Shein amefanya mambo mengi sana. Nitakapopata nafasi nitaendeleleza yale yote aliyoanza na pia  kuendeleza ikiwemo michezo." Alisema.

Hashim Salum Hashim pia ni mdau mkubwa wa michezo ambapo ameaahidi kufikisha mbali katika michezo ikiwemo kuwa Mwanachama wa Shirikisho la soka la Dunia FIFA.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.