Habari za Punde

ZEC yawataka wasimamizi wa Uchaguzi Wilaya kuvipitia kwa makini vipengele vya sheria ya uchaguzi ya mwaka wa 2020

Na Jaala Makame Haji


Tume  ya Uchaguzi ya Zanziba ZEC  imewataka wasimamizi wa Uchaguzi  wa Wilaya  kuwa makini na  kuvipitia vipengele vya  Sheria  ya Uchaguzi  no 4  ya mwaka 2018 na kanuni za uchaguzi  za mwaka 2020 ambazo zitawapatia  maelekezo  mazuri  ya  kutekeleza majukumu yao  katika kusimamia uchaguzi mkuu 2020

Makamo Mwenyekiti  wa Tume ya Uchaguzi  ZEC  MABRUK JABU MAKAME  akizugumza  wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi  na Wasimamizi wasaidizi wa Wilaya 11 za Zanzibar alisema  shughuli za Uchaguzi Mkuu  zinahitaji kuendeshwa  kwa kufuata  misingi  ya Katiba,   Sheria  na Kanuni  za Uchaguzi  ili kila mwenye haki  aweze kuipata fursa hiyo. 

waelekezeni vizuri juu ya utaratibu wa kisheria wateuliwa hao bila ya kujali ni nani amefika katika Ofisi yako kupata huduma” alisema

Alifafanua kuwa, mbali ya kuwepo kwa mafanikio makubwa  katika  kuendesha kazi za Uchaguzi katika hatua mbali mbali  ikiwemo  kazi ya Mapitio ya Majimbo ya Uchaguzi ambapo kwa sasa ni 50 badala ya 54,  uandikishaji  wa wapiga kura wapya na uhakiki wa taarifa za wapiga kura , utoaji wa vitambulisho vya Kupigia Kura lakini pia wanapaswa  kuwa  makini na  waangalifu  zaidi  katika kazi ya  utoaji wa fomu za  uteuzi wa Wagombea

 Hata hivyo, aliwasisitiza wasimamizi hao  kuhakikisha  wanafatilia kwa ukaribu kazi  ya  upigaji kura , kuhesabu  na kujumlisha  kura katika vituo  na majimbo wanayo yasimamia.

Mkurugenzi wa Uchaguzi THABIT IDAROUS FAINA alisema madhumuni ya Tume katika kuwapatia mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao katika Uchaguzi Mkuu 2020.

Akiwasilisha mada kuhusu kampeni za Wagombea Mkuu wa Kurugenzi ya Rasilimali Watu, Mipango na Uendeshaji wa ZEC SAADUN AHMED KHAMIS alisisitiza kwamba, Msimamizi wa Uchaguzi ahakikishe Mikutano yote ya kampeni za Uchaguzi katika Wilaya yake inaendeshwa katika muda na maeneo yaliyoainishwa kisheria.

Mafunzo kwa Wasimamizi na Wasimazi wa Uchaguzi wa Wilaya yanaendelea kufanyika ikiwa hatua ya utekelezaji wa mpangokazi wa uchaguzi wa kuwapatia mafunzo watendaji wote watakao husika na kazi ya usimamizi wa Uchaguzi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.