Habari za Punde

UCHAGUZI MKUU UNGEFANYIKA LEO, DK. MAGUFULI ANGESHINDA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 85 - POLEPOLE



Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndg Humphrey Polepole akiongea na wanahabari mjini Chato, mkoa wa Geita, leo Ijumaa Septemba 11, 2020

*Asema ni utafiti uliofanywa kwa kuangalia mwenendo wa kampeni siku 10 za mwanzo

*Amzungumzia Mgombea urais wa upinzani aliyekimbilia nchini baada ya mambo magumu


Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Chato
UTAFITI wa kisayansi uliofanywa na Chama Cha Mapinduzi(CCM) kupitia kitengo chake cha utafiti unaonesha kwa siku 10 ambazo Chama hicho kimekuwa kikifanya kampeni za mgombea urais wake kama Uchaguzi Mkuu ungefanyika leo Septemba 11,2020 basi Dk.John Magufuli angeshinda kwa zaidi ya asilimia 85.

Hayo yamesemwa leo Septemba 11,20202 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Humprey Polepole akiwa Chato mkoani Geita wakati akielezea mwenendo wa kampeni zao ambazo zimeendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali nchini.

"Leo tuko mkoani Geita katika Wilaya ya Chato, tunaendelea na mikutano ya kamepni ya mgombea urais na safari hii kampeni zetu zinafanywa tofauti, kampeni ya mwaka huu inafanyika kisayansi na ikizingatia weledi wa juu sana, makada waandamizi na viongozi wa ngazi mbalimbali ndani ya Chama chetu wanashambulia kila kona.

"Tuna mgombea urais na Mwenyekiti wa CCM ambaye anashambulia maeneo mbalimbali , amekutana na mamilioni ya Watanzania katika mikoa ambayo ameipata ya Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Geita, Mara,Simiyu,Mwanza na Geita.Huko ambapo amepita amekutana na mamilioni ya Waatanzania

"Pia kuna Mgombea Mwenza Mama Samia Suluhu Hassan ambaye amechukua uwanda mwingine huko Dodoma, , Morogoro, Pwani na maeneo mengine na safari hii tunatumia usafiri wa barabara, tunakwenda kijiji kwa kijiji , kata kwa kwa kata, wilaya kwa Wilaya.Mjumbe wa Kamati Kuu Kassim Majaliwa yeye amepita Dodoma,Manyara,Kilimanjaro na Arusha na safari ni ile ile Kata kwa kata, na wanaendelea kukutana na mamilioni ya watu.

"Viongozi wengine wa Chama wanaendelea kuuwasha moto kwa kuendelea na kampeni na kwa kampeni za mwaka huu ni rahisi, kuna utajiri wa kazi ambazo zimefanyika, katika kipindi cha miaka mitano na watanzana wanazielewa.Mwenyekiti mstaafu na Rais mstaafu Jakaya Kikwete anashambulia Kusini ,"amesema.

Amefafanua kampeni ni sayansi, kampeni ni mikakati,hivyo kama kulikuwa na watu wanataka kuvuruga mkoa wa Lindi , Kikwete anazifahamu vizuri siasa za mkoa huo na wamegundua mgombea mmoja(Bernard Membe) ameshaondoka nchini baada ya kuona ameshazidiwa kwa hoja.

"Na kwa taarifa ambazo tunafuatila kupitia kitengo cha utafiti, baada ya kusikia zimeshushwa silaha pale Lindi ameondoka baada ya mambo kumzidi, ni bora akakiri kuwa ameshindwa na ameingia kwenye uchaguzi kwa bahati mbaya,Mzee Kikwete anafanya kazi nzuri sana, pia yupo Mzee Mizengo Pinda ambaye kazi yake ni kufanya renki katika Kanda ya Kati akisaidiana na Job Nduga kutokana na nafasi zao dani ya Chama.

"Tutaimaliza nchi hii awamu hii yote, kisha tutapiga awamu nyingine kadhaa hivi, kwanini tunafanya yote hayo kwasababu katika kipindi cha miaka mitano tumejiimarisha, wanachama tulionao hivi sasa ni milioni 17, CCM ni wamoja zaidi kabla ya wakati mwingine wowote .

"Katika kampeni zetu awamu hii ya kwanza na tafiti za kisayansi zinazoendelea na kama kura inapigwa leo Dk.Magufuli angekuwa anashinda kwa asilimia zaidi ya 85, katika siku hizi 10 ,11, 12.Kampeni ambazo zimefanyika umma umeelewa, kimsingi nchi tumeishika na kila tunakofika nchi inasimama.Zanzibar tunakwenda vizuri mno na siku moja inayokuja tunajambo letu.

"Tutawajulisha, kazi iliyobaki ni kupiga kura tu maana kule Zanzibar wameelewa, wanataka damu changa, wanataka watu ambao wameiva kwenye uongozi.Napenda kuwambia kampeni kwa ujumla zinakwenda vizuri na kama kura inapigwa leo Septemba 11, 2020 basi Mgombea urais wa CCM Dk.John Magufuli anashinda kwa asilimia 85,"amesema Polepole na kuongeza Chama hicho kitaendelea kufanya tafiti za kampeni zake siku hadi siku kuelekea Oktoba 28 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.