Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi aongoza kikao cha kwanza cha Baraza la Mapinduzi Ikulu

 
RAIS Dk. Hussein Ali Mwinyi leo ameongoza kikao cha kwanza cha Baraza la Mapinduzi akiwa Mwenyekiti wa Kikao hicho tokea achaguliwe kwa kishindo kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, mwaka huu 2020.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Baraza la Mapinduzi Ikulu Jijiji Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi ya juu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdalla.

Wengine ni Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mawaziri, pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dk. Mwinyi Talib Haji.

Rais Dk. Hussein mwinyi, alikifungua kikao hicho na kukiongoza kama Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu cha 45 (1) inavyomtaka, ambapo  kikao hicho ni cha kwanza tokea aingie madarakani akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.