Habari za Punde

SERIKALI KUBORESHA BWAWA LA MAJI HOROHORO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga kushoto akimsaidia kufunga madumu kwenye baiskeli mmoja wa watoto aliowakuta wakichota maji kwenye bwawa la maji horohoro wakati wa ziara yake  kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly na kulia ni Meneja Ufundi wa Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shabani
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga kushoto akimsikiliza kwa umakini Mbunge wa Jimbo la Mkinga(CCM) Dastan Kitandula wakati wa ziara yake kulia ni Msimamizi wa Mradi wa Maji Horohoro kutoka Tanga Uwasa Mhandisi Salum Hamisi

SERIKALI imesema uboreshaji wa bwawa la maji la Horohoro ambalo ndio chanzo kikuu cha maji kinachotegemewa na wakazi wa mji huo uliopo mpakani mwa Tanzania na Kenya utaanza muda mfupi na utakamilika kwa wakati ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama.

Hayo yalisemwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga wakati wa ziara yake katika miradi ya maji wilaya za Tanga, Mkinga na Muheza mkoani Tanga ambapo baada ya kutembelea eneo la bwawa hilo na kupata taarifa kwamba huduma ya maji sio ya kuridhisha na ndipo alipotoa kauli hiyo.

Alisema bwawa hilo ambalo lilichimbwa na kupitia mradi wa TASAF na limekuwa  na maji ambayo kimsingi yanakuwa yakipotea licha ya kujengwa miundombinu mizuri ya kutibu maji na kusafirisha maji ikiwemo vituo vya kuchotea maji lakini bwawa  halina maji.

“Kimsingi nilipopata taarifa hizi zilinishutsha sana na nimekwisha kuwaambia wataalamu kutoka wizarani wafike eneo hilo na hivi sasa wapo njiani na nimewaambia wasiondoke hapo mpaka wampe ripoti ili ndani ya wiki mbili waweze kufanya maamuzi ya dharura ili wananchi hao waweze kuondokana na adha ya shida ya maji”Alisema

“Hatuwezi kuona wananchi wanapata shida ya maji tukatulia wakati serikali ipo na ina fedha za kujenga hiyo miradi na isitoshe tulikwisha kuwekeza na kujenga vituo vya kutibu maji na kusukuma sasa bwawa haliwezi kutushinda”Alisema Katibu huyo.

Kwa kweli inatia huruma ukiona wanajenga nyumba na nzuri mji unakuwa ila hawana maji na hapa  ni mpakani na maaeneo mengine mpakani unaweza kushangaa watu wanakosa maji wakaenda hata kutafuta nchi jirani hivyo hatutaki hilo litokee tunataka watu wa hapa wapate maji hapa hapa kwa sababu vyanzo vipi na serikali ya awamu ya tano imejipanga vizuri kuwahudumia wananchi hasa wanyonge “Alisema

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mbunge wa Jimbo la Mkinga(CCM)  Dastani  Kitandula  alimueleza katibu huyo kwamba bwawa hilo ndilo ambalo linalotegemewa kwa ajili ya kunusuru maisha ya wananchi wa vijiji vya horohoro ambapo changamoto ni kubwa ya maji
 
 Alisema kwamba wanashukuru Serikali kutoa fedha kwa ajili ya kujenga miundmbinu ya kusambaza maji lakini changamoto bado ni kubwa kwenye chanzo kuhakikisha wanazuia upotevu wa maji unaotokana na bwawa hilo kuvuja na kulipanua bwawa na kujenga tuta kubwa zaidi ili kuhakikisha wanavuna maji mengi lakini pia kuwa na uhakika maji hayatapotea.

Mbunge huyo alisema kwamba wanachokiomba kwa serikali wanajua zipo jitihada wanazofanya lakini wanaomba walichukulia jambo hilo kwa ukubwa kazi iliyofanyika ya tathmini tokea mwezi Mei mwaka huu wanaiomba yapewe kipaumbele ili kunusuru hali hiyo hata timu iliyopo njiani ikifika isiondoke mpaka ikamilisha kazi hiyo

“Kama ulivyokuja tumefarijika kwa kuona umekuja na tunaamini baada ya ziara yako hii mambo yatakuwa mazuri ili wananchi wa eneo hilo waweze kuondokana na hii changamoto ambayo  ya maji inayowakabili”Alisema Mbunge Kitandula.

Awali akizungumza Diwani Mteule wa Kata ya Horohoro (CCM) Merieyer Miliya alisema hali ya maji bado ni tatizo kutokana na kwamba maji yaliyopo kwenye chanzo ni machache na hayatoshelezi kutokana na kwamba tuta lililopo kwenye bwawa lilipasuka na kusabaisha maji kumwagika.

Alisema tatizo la maji bado ni kubwa kutokana na wananchi wengi walikuwa wakitegemea bwawa hilo na hata nchi jirani ya kenya wanategemea maji kutoka hapo kwao hivyo waliomba lipanuliwe lakini wanaamini kwa ujio wake kazi zitaanza.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.