Habari za Punde

Mbunge wa kiembesamaki akabidhi Vifaa vya kuweka Uzio katika Kituo Cha Polisi Mazizini

Na Takdir Suweid


 Mkoa wa Mjini Magharibi                                      15-01-2021.

 

Uongozi wa Jimbo la Kiembesaki umeahidi kushirikiana na Serikali zote mbili za Tanzania katika kudumisha Amani, Utulivu iliopo nchini na kuondosha Uhalifu.

 

Mbunge wa Jimbo hilo Muhammed Maulid Ali ameyasema hayo mara baada ya kukabidhi vifaa vya uwekaji wa uzio katika Kituo Cha Polisi Mazizini Wilaya ya Magharibi ‘’B’’.

 

Amesema Viongozi wakuu wa Serikali wanahubiri suala hilo hivyo watatoa michango yao ya hali na mali ili kuhakikisha malengo ya Serikali yanaendelea kufanikiwa.

 

Aidha amesema kukamilika uzio katika kituo hicho kutasaidia kutaondosha uharibifu unaofanywa na wapiti njia, Mifugo na  Mali za kituo hicho.

 

Hata hivyo amewaomba Wananchi kushirikiana na Viongozi wao ili kuweza kuwatatulia matatizo yao kwa urahisi.

 

Kwa upande wake Mkuu wa kituo cha Polisi Mazizini Salum Ameir Gayana amesema kupatikana kwa Uzio kutasaidia kunusuru upotevu wa mali, kuingia Watu na Mifugo kiholela jambo ambalo linaweza kusababisha matatizo.

 

Aidha amesema wakati uzio huo utakapo kamilika wataweza kuyaangalia mazingira yao kwa ufanisi zaidi,kutakuwa na sehemu maalum ya Watu kuingia na kutoka katika kituo hicho.

 

Nae Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai katika Jeshi la Polisi Wilaya ya Magharibi ‘’B’’ ASP Magubla amesema Msaada huo umekuja wakati muafaka kwani katika Wilaya ya hiyo kuna Vituo vingi vinavyohitaji Uzio ikiwa ni pamoja na Kijitoupele,Fumba,Mwanakwerekwe, na Fuoni hivyo amewaomba Wafadhili na Wenye uwezo kuelekeza Misaada yao

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.