Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Atembelea Kitui cha Ukusanyaji Taka Marubi na Kibele.Mradi wa ZUSP.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Uchukuaji wa taka Maruhubi Ndg. Yussuf Khamis Yussuf, akitowa maelezo ya Kituo hicho wakati wa ziara yake ya kukagua Mradi wa Huduma za Jamii Mijini (ZUSP) eneo hilo maalumu kwa ajili ya ukusanyaji wa taka zinazotoka katika eneo la mjini na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Mustafa Kitwana akitowa maelezo ya moja ya mashine ya kushindilia taka wakati zikipakiwa katika kontena katika kituo cha kukusanyika taka Maruhubi, wakati wa ziara yake kukagua Mradi wa Huduma za Jamii Mijini (ZUSP) 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akitowa agizo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Baraza la Manispa Zanzibar Ndg. Suleiman Mohammed Rashid, wakati wa ziara yake kukagua Mradi wa Huduma za Jamii Mijini (ZUSP) na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Mustafa Kitwana na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ.Mhe. Masoud Ali Mohamed
WANANCHI wa eneo la Maruhubi wakimshangilia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati akizungumza na Wananchi hao akiwa katika ziara yake kukagua Mradi wa Huduma za Jamii Mijini (ZUSP)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wananchi wakati akitembelea na kukagua Mradi wa Huduma za Jamii Mijini (ZUSP)  alipofika kukagua mtaro wa kupitishia maji katika eneo la Nyerere kwa Mtumwa jeni, akiwa katika ziara yake ilioazia kwa matembezi katika eneo la barabara ya Kiembesamaki leo asubuhi na kumalizia mnazi mmoja 27/2/2021
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wananchi wa Kwarara Madina baada ya kusikiliza kero zao wakati wa ziara yake ya kukagua Mradi wa Huduma za Jamii Mijini (ZUSP) na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana na (kushoto kwake) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said
MKAAZI wa Kwarara Madina Bi. Mwanaidi Amiri akizungumzia kero ya barabara na usafiri wa daladala wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) wakati wa ziara yake kukagua Mradi wa Huduma za Jamii Mijini (ZUSP)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Meneja wa Kituo cha Mradi wa Huduma za Jamii Mijini (ZUSP) cha utupaji wa taka Kibele Wilaya ya Kati Unguja wakati wa ziara yake kutembelea Mradi wa (ZUSP) na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Rashid Hadidi Rashid
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akitembelea eneo la utupaji wa taka katika eneo la Kibele Wilaya ya Kati Unguja akiwa katika ziara yake kukagua  Mradi wa Huduma za Jamii Mijini (ZUSP) na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Rashid Hadidi Rashid na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisikiliza kero za Wananchi wa Kibele eneo lililojengwa Kituo cha utupaji wa taka kupitia Mradi wa Huduma za Jamii Mijini (ZUSP) wakati wa ziara yake  kukagua Mradi huo na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Rashid Hadidi Rashid
Bi. Mwanaisha Abass Ali mkaazi wa Kibele akizungumza kero yake wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa ziara yake kukagua Mradi wa Huduma za Jamii Mijini (ZUSP) alipofika katika eneo la kituo cha utupaji wa taka Kibele Wilaya ya Kati Unguja leo 27-2-2021
MKUU wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Rashid Hadidi Rashid akijibu maswali yalioulizwa na Wananchi wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi katika ziara yake kukagua Mradi wa Huduma za Jamii Mijini (ZUSP) alipofika katika Kituo cha kutupa taka eneo la Kibele Wilaya ya Kati Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wananchi wa Kibele alipotembelea Kituo cha utupaji wa Taka  katika eneo la kibele akiwa katika ziara yake kukagua Mradi wa Huduma za Jamii Mijini (ZUSP) leo 27-2-2021
WANANCHI wa Kijiji cha Kibele Wilaya ya Kati Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa ziara yake kukagua eneo la Kituo cha kutupia taka Kibele, akiwa katika ziara yake kukagua Mradi wa Huduma za Jamii Mijini (ZUSP)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.