Habari za Punde

Wananchi wa Tanzania Wajitokeza Kuuaga Mwili wa Hayati Dkt.John Pombe Magufuli Ukipita Katiba Barabara ya Kawawa.Jijini Da es Salaam leo Ukielekea Uwanja wa Uhuru

Wananchi wa Kinondoni Mkwajuni na Magomeni Morocco wakiwa wamesimama barabarani kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli wakati akipitishwa katika barabara ya Kawawa kuelekea Uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Salaam kwa ajili ya kuagwa na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam.

Wajasiriamali wa Mau wa Namanga mkoani Dar es Salaam wakirusha maua kama ishara ya kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli wakati akipitishwa katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi mkoani Dar es Salaam.

Wakazi wa Biafra Kinondoni wakimuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli wakati akipitishwa katika barabara ya Kawawa.

Wakazi wa Magomeni wakimuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli wakati akipitishwa katika barabara ya Kawawa. 


Wakazi wa Kinondoni, Magomeni , Kigogo, Msimbazi Center na Karumewakiwa wamesimama kando ya barabara kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli wakati akipitishwa katika barabara ya Kawawa mkoani Dar es Salaam.
 PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.