Habari za Punde

IGP Simon Sirro Azindua Kitabu cha Muongozo wa Kifichua na Kuzuia Uhalifu.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Simon Sirro akizindua Kitabu cha muongozo wa kufichua na kuzuia uhalifu kitabu ambacho kinalenga kutoa dira hasa katika utekelezaji wa mpango wa Polisi kata kupitia mpango mkakati wa ushirikishwaji wa jamii.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka watu wanaopata msamaha wa vifungo kutoka gerezani kuacha kujihusisha na uvunjifu wa amani ikiwa pamoja na kuacha kujiingiza tena kwenye matukio ya uhalifu na badala yake wajikite katika kuleta maendeleo kwenye jamii.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati akizindua kitabu cha muongozo wa kufichua na kuzuia uhalifu kitabu ambacho kinalenga kutoa dira hasa katika utekelezaji wa mpango wa Polisi kata kupitia mpango mkakati wa ushirikishwaji wa jamii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.