Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Philip Mpanga Ahudhuria Ibada ya Pasaka Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, leo April 4,2021 amehudhuria katika Ibada ya Misa Takatifu ya kuadhimisha Sikukuu ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa Kuu Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, leo April 4,2021 amehudhuria katika Ibada ya Misa Takatifu ya kuadhimisha Sikukuu ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa Kuu Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akizungumza na Waumini wa Dini ya Kikristo na Watanzania  katika Ibada ya Misa Takatifu ya kuadhimisha Sikukuu ya Pasaka iliyofanyika leo April 04,2021 katika Kanisa Kuu Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma.
 (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amewataka Watumishi wote wa Umma na Watanzania kufanya kazi kwa Bidii, Uadilifu na weledi pamoja na  kumtanguliza Mwenyezi Mungu.

Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mpango ameyasema hayo leo April 04,2021 katika Ibada ya Misa Takatifu ya kuadhimisha Sikukuu ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa Kuu Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma.

Aidha Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kukusanya kodi kwa kuzingatia sheria za Nchi na kuwaacha Wafanya Biashara wafanye Biashara zao kwa  Haki na kutowanyanyasa kwenye Biashara zao ili kuleta kodi kwa ajili ya kuweza kuwahudumia Watanzania.

katika Ibada hiyo Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango pia amewasilisha salam za Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwaomba Waumini hao na Watanzania kwa ujumla waendelee kumuombea Rais Samia na kuiombea Nchi ili iweze kuneemeka zaidi  ya hapa ambapo Rais Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ametufikisha.

katika salamu hizo Mhe. Samia Suluhu Hassan  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawatakia Watanzania wote heri ya Sikukuu ya Pasaka na kuendelea kufanya kazi ili kuweza kuijenga Nchi yetu ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.