Viongozi wa Kamati ya kitaifa ya Maandalizi
ya UMITASHUMTA na UMISSETA wakikagua miundombinu na viwanja kwa ajili ya
mashindano hay oleo Juni 6,2021 mjini Mtwara.
1. Wanafunzi kutoka Mkoa wa Manyara wakiwasili kwenye Shule ya Sekondari ya Ufundi Mtwara leo Juni 6, 2021 tayari kushiriki mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA yatakayofunguliwa jumanne ijayo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kwenye kiwanja cha Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
1. Wanafunzi kutoka Mkoa wa Iringa wakipiga ngoma wakifurahia kuwasili leo asuburi Juni 6, 2021 tayari kushiriki mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA yatakayofunguliwa jumanne ijayo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kwenye kiwanja cha Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Na John Mapepele, Mtwara
Kamati ya kitaifa ya Mashindano
ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Sekondari (UMISSETA)
imesema leo kwamba maandalizi kwa ajili ya ufunguzi wa mashindano hayo yatakayofunguliwa
na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa
kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. Juni 8,2021 yamekamilika.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti
wa Kamati hiyo Mwalimu Ephraim Simbeye ambaye ni Mkurugezi wa Usimamizi wa Elimu
Ofisi ya Rais TAMISEMI wakati waliopotembelea leo Juni 6, 2021 kukagua miundombinu
na viwanja vitakavyotumika kwenye mashindano hayo mjini Mtwara.
“Mashindano haya yatafanyika
katika viwanja vya Nangwanda Sijaona, Chuo cha Walimu Mtwara (TTC kawaida) Chuo
cha Walimu Ufundi maarufu kama Mwasandube, na Viwanja vya Shule ya Sekondari ya
Ufundi Mtwara.” Amefafanua Simbeye
Simbeye amesema tayari mikoa
yote kutoka Tanzania Bara na Visiwani imeshaanza kuleta wanamichezo hao ambapo hadi
sasa zaidi ya wanamichezo kutoka mikoa kumi wameshawasili tayari kushiriki
mashindano hayo.
“Tunamshukuru Mungu maandalizi
yote yanakwenda vizuri na mwitikio wa ushiriki na hamasa ni kubwa, tunategemea
mambo makubwa zaidi mwaka huu” amesisitiza Simbeye
Naye Mwenyekiti Mwenza wa
mashindano hayo Yusufu Singo ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya
michezo nchini kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo amesema mashindano
haya yatasaidia kuvumbua vipaji na hivyo kupata wachezaji bora wa timu za Taifa
kwa Michezo mbalimbali
Ameishukuru Serikali kwa kushirikisha
Wizara tatu za Habari, TAMISEMI na Elimu kuratibu, kuandaa na kufanya
mashindano haya ambapo amesema kwamba huo ni mkakati mzuri utakaosaidia kukuza
sekta ya michezo kwa kasi.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Ishegoma Emmanuel Ishengoma amesema wasanii mbalimbali maarufu wa kizazi kipya, taarabu na singeli wamealikwa ili kutoa hamasa na kuwaburudisha wadau mbalimbali kwenye mashindano ya mwaka huu.
Amewataja baadhi ya wasanii
wakaokuwepo kuwa ni pamoja na Zuchu,Peter Msechu,Becka Fleva,Lina sanga Mzee
Yusufu na Dula Makabila.
Dkt. Ishengoma ametoa wito kwa wadau mbalimbali nchini kuja kujionea ubunifu na burudani kabambe itakayotolewa kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania tangia kuanzishwa kwa mashindano haya.
No comments:
Post a Comment