Habari za Punde

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Akutana na Watanzania Waliopanda Mlima Everest.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akimpongeza Balozi wa Hiari wa Mlima Kilimanjaro, Bi. Rawan Dakik kwa kuwa Mwanamke wa Kwanza Tanzania kupanda Mlima Everest  katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma jana.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) akimpongeza Mtanzania wa kwanza kupanda Mlima Everest Wilfred Moshi  katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma jana.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na  Balozi wa Hiari wa Mlima Kilimanjaro na Mwanamke wa Kwanza Tanzania kupanda Mlima Everest , Bi. Rawan Dakik (kushoto) na Mtanzania wa kwanza kupanda Mlima Everest , Bw. Wilfred Moshi (kulia) katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma jana.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (wa nne kutoka kushoto) na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (wa tatu kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na  Balozi wa Hiari wa Mlima Kilimanjaro na Mwanamke wa Kwanza Tanzania kupanda Mlima Everest Rawan Dakik (wa tatu kutoka kushoto) na Mtanzania wa kwanza kupanda Mlima Everest ,Wilfred Moshi (wa nne kutoka kulia) katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma jana. Wengine ni Wazazi wa Rawan Dakik Abdulkarim Dakik (wa kwanza kushoto), Hala Dakik (wa pili kushoto) na Mke wa Wilfred Moshi, Agnes Moshi (wa pili kutoka kulia) na Afisa Habari wa Rawan Dakik, Bw. Elifuraha Paul Mtowe.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) akimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (katikati) alipokuwa akielezea historia ya kupanda milima ya Balozi wa Hiari wa Mlima Kilimanjaro, Rawan Dakik (kushoto) na Mtanzania wa kwanza kupanda Mlima Everest, Wilfred Moshi (wa pili kutoka kushoto) katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma jana.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) akiteta jambo na Wazazi wa Rawan Dakik, Abdulkarim Dakik (wa pili kutoka kulia) na Hala Dakik (wa kwanza kushoto). Wanaoshuhudia ni Balozi wa Hiari wa Mlima Kilimanjaro, Rawan Dakik (wa pili kutoka kushoto) na Mtanzania wa kwanza kupanda Mlima Everest, Wilfred Moshi (wa tatu kutoka kushoto) katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma jana.
Picha na Happy Shayo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.