Habari za Punde

Maandalizi ya Mbio za Zanzibar International Marathon Yakamilika Kwa Asilimia Mia Moja.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akikabidhiwa Jezi kwa ajili ya Mbio za Marathon na Mwakilishi wa Kampuni ya Joma Sports kutoka Spain Zechelela Balisija akimkabidhi Jezi pamoja na vifaa vyengine, hafla hiyo imefanyika Ofisini Kwake Vuga Jijini Zanzibar.
Mwakilishi wa Kampuni ya Joma Sports kutoka Spain Zechelela Balisija akimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed namna kampuni hiyo inavyofanyakazi zake kwa karibu na waandaaji wa mashindano ya Zanzibar International Marathon.

Na.Kassim Abdi.OMPR.

Kuwepo kwa ubunifu wa mambo mbali mbali yenye maslahi na Zanzibar ni jambo jema linalokuza uzalendo kwa wananchi wake pamoja na kutanua wigo kimataifa katika kuitangaza Nchi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, alitoa kauli hiyo alipokutana  na kamati ya Zanzibar International Marathon walipofika Ofisini kwake Vuga kwa lengo la kumkabidhi vifaa vya ushiriki katika wa mashindano hayo.

Alisema ni suala la kupigiwa mfano kwa kamati ilioandaa mashindano hayo jambo ambalo limeweza kuamsha hisia kwa wadau mbali mbali wa michezo nchini.

Makamu wa Pili wa Rais alieleza suala hilo litasaidia kuitangaza Zanzibar kiutalii ambapo wageni watakaoshiriki katika mashindano hayo  wataweza kujifunza mambo mengi kutokana na upekee wa utamaduni wa kizanzibar.

Akigusia suala la ushiriki katika mashindano hayo Mhe. Hemde alitoa wito kwa wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kushiriki kwa wingi  wakifahamu kuwa michezo ni sehemu ya mazoezi na inasaidia kutengeneza Afya kimwili na kiakili.

Aidha Mhe. Hemed aliwapongeza viongozi wa kamati hiyo pamoja na  mabalozi wa ndani nan je ya nchi kwa hatua wanazozichukua kuyatangaza mashindano ya marathon.

Alipongeza Bw. Salam Kike mtangazaji wa Shika la BBC Uwengereza kwa jitihada zake akiwa kama balozi kwa kuitanga vyema Zanzibar na Tanzania kwa ujula katika anga za kimataifa.

Nae Mwenyekiti wa kamati hiyo Ndugu Hassan Suleiman Zanga alimshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa juhudi zake alizozifanya hasa katika kuwahamasisha viongozi mbali mbali sambamba na  wito wake alioutoa kwa taasisi mbali mbali nchini kuweza kuunga mkono jambo hilo, ambapo mashirika na tasisi tofauti yamejitokeza kuunga mkono.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Habari ya maandalizi ya mashindano ya marathon  Ndugu Farouk Karim alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa maandalizi ya mbio hizo kwa asilimia kubwa yameshakamilika.

Mbio hizo za Zanzibar International Marathonzinatarajiwa kufanyika  july 18 2021, ambapo hadi sasa jumla ya watu 12,000 wamekwisha kujisajili.

Wakati huo huo 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.