Habari za Punde

Mhe Jamal Kassim Ali Amekutana na Kuzungumza na Mwakilishi Mkaazi wa UNCDF Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Jamal Kassim akizungumza na  Muwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Kimataifa UNCDF Tanzania.Ndg.Peter Malika, mazungumzo hayo yaliofanyika katika Ofisi ya SMZ Jijini Dar es Salaam.me na Ujenzi wa vituo vya Dalala Zanzibar.

Na.Mwandishi Wetu.                                                                                                                                     

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Jamal Kassim(MBM)) leo amekutana na kufanya mazungumzo na Muwakilishi mkaazi wa Shirika la Umoja wa Kimataifa UNCDF , shirika linaloshughulikia masuala ya uwekezaji (mitaji) kujadili ushirikiano ya kuisaidia Zanzibar katika kuimarisha utendaji kazi wa utoaji wa huduma kwa Mamlaka ya Maji, Shirika Umeme na Ujenzi wa vituo vya Dalala Zanzibar.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika  leo katika ofisi ndogo za SMZ zilizopo jijini Dar es Salaam waziri alisema lengo la mazungumzo hayo ni kuweka mikakati ya kushirikiana katika kutekeleza miradi mbalimbali  ijnayotekelezwa na Hamlashauri na  manispaa.

Alisema katika mazungumzo  wamejadili namna ya kuzijengea uwezo manispaa, halmashauri Zanzibar ili waweze kutekeleza miradi  mikubwa ya  Masoko na Stendi za Mabasi.

Alisema Shirika hilo limekuwa likisaidia  halmashauri mbalimbali nchini Tanzania katika kutekeleza miradi mikubwa  ya  maendeleo , hivyo wanataka kutumia fursa hiyo kushirikiana nao ili waweze  kutekeleza miradi mikubwa  Zanzibar.

“Tumeona tuna fursa ya kushirikiana nao kuendeleza miradi yetu ambayo tumeiweka katika bajeti yetu, tunashukuru wametupokea na ahadi waliyotupa  sasa tutaenda kufanya  kazi pamoja ili kuhakikisha miaradi ya  mikubwa ya stendi ya mabasi, ujenzi wa masoko unaenda kuanza”  alisema.

Alisema suala  lingine ambalo wamelijadili ni uboreshaji wa miundombini  katika sekta ya maji , kuzuia upotevu wa maji, na kuboresha ukusanyaji wa mapato ya maji.

“Hili ni eneo muhimu,  litahusisha kuboresha miundombinu ya maji pamoja na kuweka mifumo  mizuri itakayodhibidi upotevu wa maji” alisema.

Alisema kwa sasa mamlaka ya maji ya Zanzibar Zawa inakabiliwa na changamoto ya mapato   kwani mapato yake mengi yanapotea  kutokana na kutokuwa na mifumo mizuri ya kukusanya mapato ya maji.

Ameeleza  suala lingine kuwa ni kuwajengea mazingira bora wajasiraiamali, , kuwajengea uwezo kwa kuwatafutia mitaji,  kuwatafutia masoko na kuwapa elimu ya biashara ili waendelee kuwa kiungo mihimu katika kukuza uchumi.

“Wajasiriamali ni sehemu muhimu  katika uchumi wa nchi yetu  kwasababu wao ndio wanaofanya mzunguko wa fedha,  wenzetu  hawa tumezungumza nao, tunataka kuja na mfumo utakaorahisisha upatikanaji wa fedha , elimu na masoko” anaeleza.

Aidha alisema Afisi ya Rais Fedha na Mipango  imejipanga kuhakikisha inatimiza malengo  ambayo serikali imejiwekea. Pia Waziri Jamali amesema wamekubaliana baada ya wiki mbili wamepanga kukutana ili kufanya makubaliano na Shirika hilo ya kusaidia kutekeleza miradi hiyo mikubwa ya maendeleo.

Nae Ndugu Peter Malika amesisitiza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kukutana  baada ya mazungumnzo hayo ya awali na wanatariajia kukutana baada ya wiki mbili  na kufanya amzungumzo ya kutekeleza miradi mikubwa ya  inayogusa maisha ya wananchi kama maji, ujenzi wa vituo vya Dalala na umeme.

“Tunaangalia miradi ya uwekezaji Zanzibar , miradi ya serikali, mashirika ,  miradi ya  halmashauri hasa miradi ya kusambaza maji, umeme na ile unayowagusa wananchi “  alisema.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.