Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Atembelea Eneo la Mradi wa Ujenzi wa Matangi ya Maji Kwarara Kidutani Akiwa Katika Ziara Yake Wilaya ya Magharibi "b" Unguja.

Eneo linalojengwa matangi Matatu ya kusambazia maji katika maeneo ya Mji wa Zanzibar Kwarara Kidutani Wilaya ya Magharibi "B" Unguja likiendelea na ujenzi huo unaofanywa na Kampuni ya L&T Construction kutoka Nchini India kupitia Mradi wa Benk ya Exim.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Idrisa Kitwana Mustafa akizungumza wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa katika ziara yake kutembelea miradi ya maendeleo katika Mkoa huo. Akiwa katika eneo la Mradi wa Maji wa Exim Bank Kwarara Kidutani Wilaya ya Magharibiu "B" Unguja. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Dkt.Salha Mohammed Kassim akitowa maelezo ya Kitaalum ya Mradi wa Ujenzi wa Matangi ya kusambazia maji kupitia Mradi wa Maji wa  Exim Bank, katika eneo la Kwarara Kidutani Wilaya ya Magharibi "B" Unguja.

Meneja Msimamizi Mradi wa Ujenzi wa Matangi ya Maji Kwarara Kidudani kutoka Kampuni ya L&T Construction ya India Ndg. Harshaverdhan akitowa maelezo ya maendeleo ya Ujenzi huo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati alipotembelea Mradi huo akiwa katika ziara yake Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wakandarasi wa Mradi wa Ujenzi wa Matangi ya Maji katika eneo la Kwarara Kidutani, wakati alipofika kutembelea Mradi huo wa Exim Bank wa Uchimbaji wa Visima na ujenzi wa Matangi ya kusambazia maji katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar, wakati wa ziara yake katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Wakandarasi wa Kampuni ya Ujenzi wa Matangi ya Maji ya  L&T Construction kutoka India  wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) wakati akitembelea Mradi wa Maji wa Exim Bank  wa ujenzi wa Matangi na uchimbaji wa Visima vipya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Aliu Mwinyi akitembelea eneo la Mradi wa Ujenzi wa Matangi ya Maji na Visima katika eneo la Kwarara Kidutani Wilaya ya Mjini Unguja akiwa katika ziara yake katika Mkoa wa Mjini Magharibi "B" Unguja. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.