Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais, Mhe Hemed afanya ziara ya kushtukiza hospitali ya Mwembeladu na Hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongo chekundu

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akimuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi Moja kuhakikisha Vita tiba na Dawa muhimu zinapatikana kwa wakati katika Hospital Mbali mbali Nchini wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Hospital ya Mwembeladu.
Mmoja ya wananchi waliofika katika Hospitali ya Mwembeladu akimueleza Makamu wa Pili wa Rais changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo kukosekana kwa kipimo cha damu katika Hospital hiyo.
Mhe. Hemed akizungumza na wananchi waliofika kupata huduma katika Hospital ya Mwembeladu huku akiwaelezea azma ya serikali ya awamu wa nane katika kutatua changamoto za sekta ya Afya kwa ajili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi wake.
Mhe. Hemed akizungunza na wananchi waliofika kupata huduma katika Hospital ya Mwembeladu huku akiwaelezea azma ya serikali ya awamu wa nane katika kutatua changamoto za sekta ya Afya kwa ajili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi wake.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akikagua maeneo mbali mbali katika Hospital ya wagonjwa wa akili ya Kidongochekundu kufuatia ziara ya kushtukiza alioifanya leo kwa ajili ya kujionea huduma zinazotolewa kwa wananchi.


Na Kassim Abdi, OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameutaka uongozi wa Wizara ya Afya kutatua changamoto ya kukosekana kwa Vifa tiba katika Hospital na vituo vya Afya Nchini Ili kurahisisha upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.

Mhe. Hemed alileza hayo kupitia ziara ya kushtukiza alioifanya katika  hospitali ya Mwembeladu na Hospital ya Wagonjwa wa akili kidongoChekundo kwa lengo la kujionea huduma zinavyotolewa kwa wananchi wanaofika katika spitali hizo.

Alisema viongozi wenye dhamana ya kusimamia vituo vya Afya wana jukumu la kuhakikisha vifaa tiba vinavyohitajika vinapatikana kwa wakati sambamba na kufanya ukarabati wa meneo mbali mbali ili kuweka mazingira bora kwa wafanya kazi wanaotoa huduma kwa wananchi.

Akitembelea spital ya Mwembeladu Makamu wa Pili wa Rais alisema maeneo ya kufanyia kazi kwa madktari katika spital hiyo sio ya kuridhisha, hivyo amemuagiza Mkurgenzi Mtendaji wa Hospital ya Mnazi Moja Dk. Msafiri Marijani kuchukua hatua za haraka kwa kufanya ukarabati wa kawaida katika baadhi ya maeneo.

Akikagua sehemu ya kuhifadhia dawa na vifaa tiba Mhe. Hemed alimuelekeza Dk. Marijani kuhakikisha vifaa tiba ikiwemo mikoba ya kujifungulia pamoja na dawa muhimu zinazopatikana katika bohari kuu ya serikali zinapatikana kwa wakati katika spital hizo.

Nao, Wafanyakazi wa hospital hiyo ya Muembeladu walimuomba Mhe. Hemed akiwa mtendaji mkuu wa shughuli za serikali kuzipatia ufumbumbuzi changamoto zinazowakabili ikiwemo uchakavu wa jengo pamoja na upungufu wa wafanyakazi kwa ajili ya kutoa huduma katika chumba cha upasuaji.

Mara baada ya kukamilisha ziara yake katika Spital hiyo ya Mwembeladu Makamu wa Pili wa Rais alitoa furasa kwa wananchi waliofika kupata huduma spitalini hapo  kuelezea changamoto wanazokabiliana nazo na kueleza kuwa, wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa kipimo cha Damu hali inayosababisha usumbufu kwa kugharamika kutoa fedha ili kupata kipimo hico Nje ya Hospital hiyo.

Akizungumza na wananchi hao Makamu wa Pili wa Rais alisema serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Rais Dk. Hussein Mwinyi imedhamiria kutatua changamoto katika sekta Afya ili kuwapatia huduma bora wananchi wake.

Wakati huo huo, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amefika katika Hospitali ya wagonjwa wa akili ya kidongochekundu na kukagua maeneo mbali mbali yanayotolewa huduma kwa wagonjwa.

Akiwa katika eneo hilo Mhe. Hemed ametembelea katika sehemu maalum za kumpuzikia wagonjwa hao ili kujionea mazingira halisi na aliwagiza wafanyakazi kuendelea kutoa huduma kwa walengwa na kutokata tamaa kutokana na changamoto wanazokabiliana nazo.

Katika ziara yake hiyo, Makamu wa Pili wa Rais ametembelea jengo jipya linalotarajiwa kutoa huduma kwa wagonjwa na kuitaka kampuni ya RANS kukamilisha ujenzi huo ili kutoa fursa ya kutumika kwa jengo hilo ili kutatua changamoto ya ufinyu wa nafasi kwa wafanyakazi.

Kabla ya kuhitimisha ziara yake, Mhe. Hemed alipata fursa ya kuzungumza na waathirika wa madawa ya kulevya wanaopata matibabu kituoni hapo na kuwapongeza kwa uamuzi wao wa kuachana na vitendo hivyo vya utumiaji wa madawa ya kulevya.

Alisema katika kuhakikisha serikali inawaunga mkono kuachana na vitendo hivyo imepitisha bajeti ya Zaidi ya Billioni Themanani kwa ajili ya kuwawezesha kwa kuwapatia mitaji na mafunzo ya ujasiriamali kwa lengo la kuendesha maisha yao.

Aliwataka waathirika hao walioamua kuacha kwa hiyari matumizi ya madawa ya kulenvya kutorudia tena katika vitengo hivyo kwani serikali inawategemea kwa ajili ya kutoa mchango wao katika ujenzi wa Taifa.

Nae, Rais wa Waathirika wa madawa ya kulevya Ndugu Ibrahim Mrisho Mohamed alipongeza serikali kwa jitihada zao kutokana na huduma bora wanazopatiwa kituoni hapo na kuiomba serikali kuwapatia nafasi za ajira ili wasirudie tena katika matumizi haramu ya madawa ya kulevya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.