Habari za Punde

Wahasibu Wanawake Tanzania (TAWCA) Wapongezwa kwa Jitihada Zao Kuandaa Viongozi Bora.

Mwenyekiti wa Chama cha Wahasibu wanawake Dk. Neema Kiule akisoma taarifa fupi ya Chama chao ambapo alimueleza Mgeni rasmi kuwa Chama chao kimetoa mchango mkubwa kwa Jamii kwa kuwawezesha wajasiriamali wanawake wapatao 101 kuemndesha biashara zao ndogondogo.
Mhe. Hemed akizungumza na wanachama wa Chama cha Wahasibu wanawake Tanzania (TAWCA) katika Kongamano la Nne la Chama hicho lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hotel Verde Mtoni ambapo Mhe. Hemed alimuwakilisha Rais Dk. Mwinyi.
Washiriki wa Kongamano la Chama cha wahasibu wanawake Tanzania wakifuatilia Hotuba ya Mgeni wakatika akilifungua Rasmi Kongamano la Nne la Chama cha Wahasibu wanawake Tanzania liliolofanyika katika Mkumbi wa Mikutano wa Hotel Verde Mtoni.
Washiriki wa Kongamano la Chama cha wahasibu wanawake Tanzania wakifuatilia Hotuba ya Mgeni wakatika akilifungua Rasmi Kongamano la Nne la Chama cha Wahasibu wanawake Tanzania liliolofanyika katika Mkumbi wa Mikutano wa Hotel Verde Mtoni.

Na.Kassim Abdi. OMPR.                                                                               

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Hussein Ali Mwinyi amekipongeza Chama cha Wahasibu Wanawake Tanzania (TAWCA) kwa jitihada zao katika kuandaa viongozi bora wanawake wanaotoa mchango kwa maendeleo ya Taifa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alieleza hayo kupitia Hotuba alioisoma kwa niaba ya Rais Dk. Huseein Mwinyi katika ufunguzi wa kongamano la nne la uongozi la wanawake wahasibu Tanzania (TAWCA) lililofanyika katika ukumbi wa Hotel Verde Mtoni Jijini Zanzibar.

Mhe. Hemed alisema amefurahishwa na mikakati iliowekwa na chama hicho katika kuhakikisha wanalisaidia taifa kwa kuandaa viongozi mbali mbali wanawake ambao wamekuwa wakitoa mchango wao katika kukuza Uchumi wa Nchi.

Alieleza kuwa Serikai ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kuthamini mchango wa chama hicho kutokana na kufanya kazi nzuri katika kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika kujitolea na kuleta maendeleo Nchini.

Makamu wa Pili wa Rais alisema kwamba Tanzania ina viongozi wengi wakupigiwa mfano ambao wameweza kushika nafasi mbali mbali kitaifa na kimataifa, kutokana na uwezo walionao wao. jambo ambalo limetoa Imani kubwa kwa jamii kwa viongozi wanawake.

Alifafanua kuwa, Serikali kutokana na mchango mkubwa waliouonesha kwa Taifa aliwahakikishia kuwa serikali ya awamu ya nane itaendelea  kuwaamini wanawake kwa kuwapa fursa mbali mbali za Uongozi.

Pia alisema Chama cha Wahasibu wanawake kimekuwa na mchango mkubwa katika kujenga uchumi wa nchi kutokana na utaalamu wao pamoja na kuwa na mipango mizuri ya kuimarisha ustawi wa sekta mbali mbali ikiwemo Uhasibu.

Kupitia Hotuba hiyo Mhe. Hemed  aliwaasa wahasibu hao kuendelea kuwashawishi na kuwahamasisha wanawake wengi Zaidi kujiunga na elimu ya juu kwa kusomea fani hiyo, ili miaka ya mbele nchi iwezze kuwa na wataalamu wengi wanawake ambao taifa linatagemea kwa kiasi kikubwa mchango wao.

Pamoja na mambo mengine Makamu wa Pili wa Rais aliwataka washiriki hao kuunga mkono jitihada zinazochukuliwa na  Serikali zote mbili katika  kupiga vita rushwa pamoja na vitendo vya ubadhirifu wa fedha za umma.

Nae, Mwenyekti wa Chama cha Wahasibu Wanawke Tanzania Dk Neema Kiure Msussa, alieleza kuwa Chama hicho kimesajiliwa mwaka 2015 ambapo hadi sasa kina jumla ya wanachama 730.

Alieleza kuwa, TAWCA  katika kuwawezesha wajasirimali wanawake imesaidia jumla ya wanawake 101 kwa kuwapatia elimu pamoja na kuwapa mafunzo na mitaji kwa ajili ya kuimarisha harakati zao za kimaisha kupitia biashara.

Alieleza kwamba chama hicho kimetanua wigo kitaifa na kimataifa kwa kujiunga na vyama mbali mbali vya wahasibu wakiwa na lengo la kupata uzoefu kutoka kupitia wataalamu tofauti kutoka mataifa mengine.

Akiwasilisha salamu kutoka Hospitali ya Agakhan katika kongamano hilo Dk. Erine Kitege alieleza kuwa katika Kongamano hilo wataalamu kutoka Hospital hiyo watafanya vipimo vya saratani ya Shingo ya kizazi na saratani ya matiti kutokana na kina mama kukumbwa na ugonjwa huo.

Dk. Kitege alieleza kuwa asiliamia 75 ya kina mama hawafiki hospitali kwa wakati kupata huduma ya tiba ya saratani  jambo ambalo linapelekea kuleta athari za kiafya kwa akina Mama.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.