Habari za Punde

Benki ya CRDB Yakabidhi Cheti cha Udhamini wa Mjadala wa Uwekezaji Zanzibar The Big Breakfast.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Cheti cha Udhamini Mjadala wa Uwekezaji Zanzibar Big Breakfast Meneja Uhusiano Bima Benki ya CRDB -Zanzibar Bi.Hamida Juma, wakati wa hafla hiyo iliyowajumuisha Wadau wa Uwekezaji Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar. jana 24-9-2021. 
Maofisa wa Benki ya CRDB wakifuatilia kwa makini Mjadala wa Uwekezaji Zanzibar wakati ikiwasilishwa Mada kuhusiana ya Fursa za Uwekezaji Zanzibar ikiwasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA  Zanzibar Bw. Shariff Ali Shariff.(hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya Wadhamili wa Mjadala wa Uwekezaji Kiuchumi Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.