Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais, Mhe Hemed akutana na Balozi mdogo wa Oman

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na Balozi mdogo wa Oman SAID ALSINAWI aliefika Afisini kwake Vuga kujitambulisha ambapo Mhe. Hemed ametumia fursa hiyo kumueleza fursa zilizopo Zanzibar kupitia uwekezaji ikiwa azma ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekusudia kukuza uchumi wake kupitia Uchumi wa Buluu.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akipata picha ya pamoja na  Balozi mdogo wa Oman SAID ALSINAWI aliefika Afisini kwake Vuga kujitambulisha ambapo Mhe. Hemed ametumia fursa hiyo kumueleza fursa zilizopo Zanzibar kupitia uwekezaji ikiwa azma ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekusudia kukuza uchumi wake kupitia Uchumi wa Buluu.

Na Kassim Abdi OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendeleza uhusiano na ushirikiano wake na Oman kwa maslahi ya wanachi wake baina ya pande mbili.

Mhe. Hemed ameeleza hayo Afisini kwake Vuga alipokutana na Balozi Mdogo wa Oman SAID ALSINAWI alipofika kwa ajili ya kujitambulisha.

Amesema Serkali ya Mapinduzi Zanzibar inathamini ushirikiano wa kihistoria uliokuwepo kwa muda mrefu ambapo Oman imekuwa ikiunga mkongo Zanzibar kupitia sekta mbali mbali ikiwemo kuimarisha elimu kwa wananchi wa Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais alimueleza Balozi huyo wa Oman anaefanyia kazi zake Zanzibar kuwa, Wakati umefika kwa nchi hiyo kuja kuekeza Zanzibar ikizingatiwa kwa sasa Zanzibar imejikita kukuza uchumi wa ke kupitia sekta ya Uchumi wa Buluu (Blue Economy).

Katika mazungumzo yao, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimuhakikishia Balozi SAID ALSINAWI kumpatia ushirikiano wa karibu wakati akitekeleza majukumu yake hap Zanzibar.

Nae, Balozi mdogo wa Oman SAID ALSINAWI alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nchi ya Oman itaendelea kushirikiana na Zanzibar kutokana na uhusiano wake wa kidugu wa miaka mingi iliopita.

Kuhusu suala zima la Uwekezaji, Balozi SAID ALSINAWI alisema Oman tayari imeonesha nia yake ya kuekeza Zanzibar kupitia sekta mbali mbali ambapo kwa sasa mipango hiyo  ipo katika machakato.

Alieleza kwamba, Ujio wa Ndege yao ya Oman Air ikiwa imebeba abiria wa kutosha kwa safari zake hapa Zanzibar ni kielelezo tosha cha ushirikiano baina ya nchi mbili hizo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.