Habari za Punde

UVCCM Mkoa wa Kusini Unguja Wapongezwa kwa Kuazisha Program ya Inayolenga Kuwasaidia Katika Mkoa Huo.

Vijana wa UVCCM Mkoa wa Kusini wakimvisha Skafu Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati alipowasili katika Ukumbi wa Mikutano wa TC Dunga kwa ajili ya uzinduzi wa Programu ya Elimu ilioandaliwa na UVCCM Mkoa wa Kusini.
Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na wanachama wa CCM na viongozi mbali mbali katika shughuli ya uzinduzi wa Programu maalum ya kuinua Elimu Mkoa wa Kusini Unguja hafla iliofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Walimu Dunga.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akipokea Computer Kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Uzini ambape Pia ni Naibu waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Khamis Hamza Chilo ikiwa ni miongoni mwa Vifaa alivyovitoa Mbunge huyo katika jitihada za kuunga mkono Programu ya Elimu ya UVCCM Mkoa wa Kusini.
Mhe. Hemed akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadidi Rashid Fedha Taslimu zilizochangwa na viongozi kwa kushirikiana na wanachama wengine kwa ajili ya kusaidia Programu ya Elimu ilioandaliwa na UVCCM Mkoa wa Kusini ambapo katika Harambee hiyo ndogo ilioendeshwa zimekusanywa Jumla ya shiliingi Millioni Kumi (10,000,000/=).
Na.Kassim Abdi.OMPR.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmshauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameupongeza Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja kwa kuanzisha Program ya elimu ya inayolenga kuwasaidia wanafunzi ndani ya mkoa huo.

Mhe. Hemed ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitoa pongezi hizo katika uzinduzi wa Program ya elimu ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja iitwayo “kuza ufaulu” hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kituo cha Walimu Dunga Mkoa wa Kusini Unguja.

Alisema suala la kukuza ufauli kwa wanafunzi ni jambo la msingi ikizingatiwa kuwa Mkoa wa Kusini Unguja kitakwimu ni Mkoa ambao matokeo yake hayaridhishi ndani ya miaka miwili mfululuzo.

Alieleza matarajio ya Program hiyo ni kuleta mabadiliko endelevu ambayo itatoa fursa kwa vijana wanaoendelea na masomo yao hasa ya katika elimu ya sekondari kuweza kukuza uelewa wao wa masomo na hatimae kuweza kuwa mfano kwa taifa katika ufaulu wao.

Alisema umefika wakati sasa kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi katika ngazi zote kutoa mashirikiano ya kila hali ili kuhakikisha azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kukuza elimu kwa hatua ya kupunguza ziro na kukuza ufaulu inaweza kufikiwa.

Mhe. Hemed alisema si jambo la kuridhisha kwa Mkoa huo kuwa ni wa mwisho kielemu ukizingatia katika masuala mengine mbali mbali Mkoa huo ni wa kupigiwa mfano hasa uwepo wa nyenzo za kutosha kushawishi watoto kuweza kufanya vyema kwenye masomo yao.

Akigusia kuhusu malezi Mheshimiwa Hemed alieleza ni vyema kushirikiana pamoja katika malezi ili vijana waweze kufikia malengo yao ya kutafuta elimu.

“Naomba niwatanabahishe kuwa nidhamu kwa wanafunzi ni msingi wa mafanikio” Alieza Mhe. Hemed.

Pamoja na mambo mengine, Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa ameendelea kuwataka voingozi wa Chama na Serikali kuelekeza nguvu zao katika kusaidia kukuza sekta ya elimu ili kuisaidia Serikali katika kuwahudumia vijana hao.

Mhe. Hemed alieleza kuwa, Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi imeweka mipango thabiti katika kuinua sekta ya elimu nchini ili wananchi wake waweze kupata elimu bila ya kikwazo chochote.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja Ndugu Muhamed Ali Muhamed alisema kuanzisha Program hii  inatokana na hali ya elimu kushuka ndani ya mkoa huo.

Alieza kwamba, katika kuelekea zoezi la sensa ya watu na makazi Umoja wa Vijana unaendelea kushajiihisha vijana kushiriki katika zoezi hilo, ili kusaidia kurahisha kuleta maendeleo kwa wananchi wake ambapo kupitia sensa hiyo sekta ya elimu itapata msukumo wa kufikisha huduma kwa vijana kwa urahisi

Kwa upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Simai Muhamed Said alisema Wizara imeweka mkakati madhubuti wa kuhakikisha changamoto mbali mbali katika sekta ya elimu zinatatuliwa ili kufikia malengo yaliokusudiwa.

Alieleza Wizara imefurahishwa kwa kuanzisha  Program hiyo  ambayo itaweza kusaidia kukuza ufaulu, na kuwataka wazazi na walezi kuwa karibu zaidi na walimu pamoja na wasimamizi wa program hiyo ili kuwatia nguvu kwa lengo la kuwasaidia watoto hao.

Akisoma risala Katibu wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Kusini Unguja Ndugu Aboud Said Mpate amesema kuwa Program hiyo kwa kuanzia  imelewanga wanafunzi wa Skuli tano wanaotarajiwa kufanya mitihani kidato cha nne pamoja na kidato cha pili zilizokuwepo katika Majimbo ya Mkoa wa Kusini.

Katika hafla hiyo ya Uzinduzi Mjumbe huyo wa Kamati kuu ya CCM Taifa Mhe. Hemed alishajihisha mchango maalum ambapo jumla ya shilling Millioni Kumi zilichangwa ikiwemo fedha taslim pamoja Ahadi pamoja na chakula na kitoweo kitakachowasaidia wanafunzi waliopo katika makambi ya skuli ndani ya Mkoa huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.