Habari za Punde

Benki Kuu ya Tanzania ( BoT) Yapongeza Mfumo wa Majaribio ya Suluhishi za Kidigitali NMB

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dk. Bernard Kibesse , Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin Mhede(kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna na Kaimu Afisa Mkuu Teknolojia na Mabadiliko ya Kidigitali wa NMB, Kwame Makundi wakipata maelezo ya suluhishi mbali mbali za mifumo ya kifedha ya tehama kutoka kwa mmoja wa wakilishi wa kampuni changa ya tehama, katika uzinduzi wa mfumo wa majaribio ya kidigitali wa NMB.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dk. Bernard Kibesse , Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin Mhede, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna na Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa NMB, Benedicto Baragomwa, wakipata maelezo ya suluhishi mbali mbali za mifumo ya kifedha ya Tehama kutoka kwa mmoja wa wakilishi wa kampuni changa ya tehama katika uzinduzi wa mfumo wa majaribio ya kidigitali wa NMB.

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dk. Bernard Kibesse , Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin Mhede (kati kati) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna wakipata maelezo ya suluhishi mbali mbali za mifumo ya kifedha ya Tehama kutoka kwa mmoja wa wakilishi wa kampuni changa ya tehama, katika uzinduzi wa mfumo wa majaribio ya kidigitali wa NMB.

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dk. Bernard Kibesse , Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin Mhede (kati kati) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna wakizungumza mara baada ya uzinduzi wa mfumo wa majaribio ya kidigitali wa NMB.

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dk. Bernard Kibesse akizungumzza wakati alipozindua mfumo wa majaribio ya kidigitali wa NMB.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin Mhede mfumo wa majaribio ya kidigitali wa NMB.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna akizungumza katika uzinduzi wa mfumo wa majaribio ya kidigitali wa NMB.
Mhazini wa Benki ya NMB, Aziz Chacha(kushoto) na Afisa Mkuu wa Rasilimali Watu wa NMB Emmanuel Akonaay, ni miongoni ya waliohudhuria uzinduzi wa mfumo wa majaribio ya kidigitali wa NMB uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City – Dar es Salaam.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dk. Bernard Kibesse akiteta jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna kulia na Mkuu wa kitengo cha Biashara za Serikali cha NMB – Vicky Bishubo mara baada ya uzinduzi wa mfumo wa majaribio ya kidigitali wa NMB.

Benki ya NMB imezindua Mfumo wa Majaribio ya Suluhishi za Kidijitali (Sandbox Environment), ikiutengea Sh. Bilioni 1 za kusaidia bunifu zitakazopita, Mfumo ambao umepongezwa na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Bernard Kibesse, na kutaka Taasisi za Fedha nchini kuiiga NMB katika kuleta njia mbadala za kutoa suluhu za kibenki ambazo ni rahisi, haraka na salama.

NMB Sandbox ni jukwaa huru la NMB linalotoa fursa kwa wabunifu wa Kidogitali na wabunifu binafsi wa Kitanzania kutumia Mifumo ya benki ya NMB kujaribu suluhishi zao kabla ya kuanza kutumika rasmi.

Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam, ambapo Mgeni rasmi Dk. Kibesse alisisitiza kuwa mabenki nchini hayana budi kuendana na kasi ya mabadiliko ya tekinolojia ili kutoa suluhishi za huduma za kibenki, hasa katika nyakati hizi, ambazo tekinolojia imetanua wigo wa kuhudumia.

“Uzinduzi huu wa Sandbox Environment, unafungua fursa kwa Kampuni changa na wabunifu binafsi kuonyesha ujuzi wao na kubuni suluhishi zitakazopunguza gharama za kibenki kwa watu wote, sambamba na kutengeneza ajira kwa vijana wa Kitanzania.

“BoT inatambua changamoto zinazo wakabili wateja wanapotumia huduma za kibenki, zikiwemo upatikanaji hafifu wa huduma hizo, ufinyu wa njia za kufikisha, gharama na uelewa mdogo walionao katika masuala ya fedha.

“Serikali kupitia BoT imechukua hatua mbalimbali kumaliza changamoto hizo na uzinduzi huu unaashiria kuwa NMB inaunga mkono jitihada hizo, Kama ilivyofanya kutenga Sh. Bilioni 100 za mikopo nafuu kwa wakulima, wafugaji na wavuvi,” alisema Dk. Kibesse, akiahidi kuwa BoT itaendelea kushirikiana na NMB katika kuboresha sera zinazotoa mwongozo na kurahisisha ufanyaji wa biashara kwenye sekta ya kibenki.

Awali, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, alisema benki yake imejidhatiti na kujipambanua kuendana na kasi ya tekinolojia kwa kuleta suluhishi mpya zinazorahisisha huduma za kibenki kwa mteja mmoja mmoja na wafanya biashara wadogo na wa kati, na kwamba benki yake imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 1 kwa ajili ya kuziwezesha suluhishi zitakazopita katika majaribio hayo.

Zaipuna alimhakikishia Dk. Kibese kuwa, licha ya kwamba utatumika kwa majaribio, lakini Sanbox Environment hautoathiri kwa namna yoyote usalama wa taarifa, amana na faragha za wateja wao na kwamba baadhi ya tuzo za miaka ya karibuni ilizopata benki hiyo zimetokana na uwekezaji mkubwa waliofanya katika mifumo ya Kidijitali.

“Hivi karibuni tumeshinda Tuzo ya Benki Bora ya Ubunifu ya wateja binafsi kutoka Jarida la Kimataifa la International Banker, huku tukiendelea kuongoza sokoni katika kutoa huduma za kibenki kidijitali na kuongeza bunifu Kama hizi za kuwaleta karibu wateja wetu kupitia mifumo ya kiteknolojia.

“Tunaahidi kuendelea kuongeza juhudi za kuhakikisha tunafikisha na kuchagiza matumizi ya huduma za kifedha miongoni mwa Watanzania bila kujali walipo, yote yakiwezeshwa na bunifu hizi za Kidijitali,” alisema Zaipuna na kubainisha kuwa Sandbox Environment ni jukwaa muafaka kwa Kampuni za Ubunifu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kufanya majaribio ya bunifu zao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.