Habari za Punde

Ashikiliwa na Polisi kwa kukutwa na mali zinazomilikiwa na kampuni ya Masterlife

Na Kijakazi Abdalla      Maelezo   7/12/2021

MWENYEKITI wa kamati ya Masterlife ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamalaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar (ZAECA),Ahmed Khamis Makarani amesema mtu mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kukutwa na mali zinazomilikiwa na kampuni ya masterlife.

 

Mwenyekiti alisema hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari katika ukumbi wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Vuga Mjini Unguja.

 

Mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Peter Abel mkaazi wa Dares esalam anadhibitiwa na vyombo vya sheria ili arejeshe mali hizo na akikataa hatua zaidi zitachukuliwa ili kuhakikisha Serikali inasimamia haki na maslahi wa wananchi wake.

 

Alisema kuna orodha ya mara ya pili ambayo inatarajiwa kutolewa lakini kuna baadhi ya watu hawatokuwemo katika orodha hiyo na badala yake waende katika ofisi za mamlaka ya rushwa kwa ajili ya kuangalia majina yao.

 

Nae Kamishna wa Bajeti Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Saumu Khatib Haji, alisema tayari wameshatoa orodha ya majina ambao wanastahiki kwa awamu ya kwanza ambapo watalipa kupitia benki kwa kutoa namba yake ya akaunti atakapofika eneo la malipo na alokuwa hana atafanyiwa utaratibu wa kufungua ili kuruhusu wote kulipwa katika mfumo mmoja.

 

Aidha alisema wameanza na wananchi waliowekeza kiwango kidogo na baadae zoezi hilo litakwenda kwa wananchi wa awamu ya pili.

 

Alisema kwa awamu ya pili wameanza na utaratibu kwenda kuangalia majina yao ambapo tarehe 13 mwezi huu yatabandikwa katika Ofisi zote za wakuu wa mikoa kwa Unguja na skuli ya Haile selasie.

 

Alisema watakaoona majina yao watakwenda holi la Haile kwa ajili ya kutambuliwa na kwa awamu hii hakutolipwa bila ya kutokuwa na namba ya benki.

 

Aliwasisitiza wananchi ambao wamo katika hatua hiyo kuhakikisha kwamba wanakwenda na vielelezo muhimu ikiwemo mkataba wake original, kitambulisho cha Mzanzibari mkaazi au Mtanzania alichotumia wakati wa usajili wa kuweka fedha na picha moja ya paspoti saizi.

 

Alisema hatua hiyo inatokana na kauli ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kuwahakikishia wahanga hao kila mmoja anapatiwa haki yake.

 

Aliwasisitiza wananchi kuhakikisha wanafuata maelezo na taratibu zilizowekwa katika zoezi hilo kwa kuchukua vitu vyao vyote ili waweze kupatiwa amana yao.

 

Sambamba na hayo alisema Serikali inaendelea kupiga mnada vitu vyote

 

Alisema wanatambua kwamba jambo hilo lilileta taharuki kubwa kwa wahanga waliowekeza fedha zao katika kampuni hiyo.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi wakati akilihutubia taifa katika mwaka mmoja wa uongozi wake alisema kampuni hiyo ilikusanya kiasi cha shilingi bilioni 38.7 kwa wananchi 10,317 wengi wao wakiwa ni wananchi wanyonge na kusema kwamba serikali imefanya uamuzi wa kuwalipa wananchi hao amana zao.

 

Hata hivyo alisema wanataka kuhakikisha kwamba hadi ifikapo Disemba 23 mwaka huu watu wote wawe washalipwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.