Habari za Punde

Mwenyekiti wa TRFA Aishukuru Kampuni ya Ruby International Kwa Kudhamini Ligi ya Mkoa.

 

    MWENYEKITI wa Chama cha Soka Mkoa wa Tanga (TRFA) Saidi Soud katika akizungumza kuhusu udhamini walioupata kutoka kwa Kampuni ya Ruby International inayojihusisha na uchumbaji madini kulia ni Katibu wa TRFA Beatrice Mgaya na kushoto ni Mwakilishi wa Kampuni ya Ruby International Thomas Machupa.

Mwakilishi wa Kampuni ya Ruby International Thomas Machupa akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tanga (TRFA) Saidi Soud na kulia ni Katibu wa TRFA Beatrice Mgaya

Mwakilishi wa Kampuni ya Ruby International Thomas Machupa kushoto akimkabidhi kombe litakaloshindaniwa kwenye fainali ya Ligi ya Mkoa wa Tanga Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tanga (TRFA) Said Soud kulia anayeshuhudia ni Katibu wa TRFA Beatrice Mgaya

Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tanga (TRFA) Said Soud kushoto akimkabidhi Kombe hilo  Katibu wa TRFA Beatrice Mgaya mara baada ya kukabidhiwaNA OSCAR ASSENGA, TANGA.

MWENYEKITI wa Chama cha Soka Mkoa wa Tanga (TRFA) Saidi Soud ameishukuru Kampuni ya Ruby International inayojihusisha na uuuzaji na uchumbaji wa madini nchini kwa kuona umuhimu wa kudhamini ligi ya mkoa huo.

Akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari Soud alisema udhamini huo utasaidia kuongeza ushindani na tija kubwa kwenye Ligi hiyo ambayo huchezwa kila mwaka .

Alisema licha ya udhamini huo kuongeza ushindani lakini pia utakuwa ni chachu ya kuibua vipaji vipya kwa vijana kupitia mpira wa miguu ambao baadaye kupitia timu za ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Alisema hatua ya kumpata mfadhili huyo ni jambo ambalo limeweka historia kwa soka la Tanga ambayo sasa inakwenda kukiinua chama hicho pamoja na kuboresha michuano hiyo .

“Lakini kikubwa niwashukuru kampuni hii ya Ruby International kwa kuona umuhimu wa kudhamini ligi hii hivyo niwahakikishie kwamba tutahakikisha tunashirikiana nao bega kwa bega”Alisema

Awali akizungumza katika Mwakilishi wa Kampuni ya Ruby International Tom Machupa alisema watazidi kufanya mambo makubwa zaidi kwa ajili ya kukuza vipaji na kuipa hadhi ligi hiyo.

Machupa alisema wao kama kampuni ya Ruby watahakikisha wanashirikiana nao ili wazidi kufanya mambo makubwa kwenye Ligi ikiwa ni kukuza vipaji na kuipa hadhi ligi hiyo


Ligi hiyo inashirikisha timu 16 kutoka wilaya zote 8 za mkoa wa Tanga kila msimu ambapo msimu huu itakwenda kufikia tamati January 2, 2022 itakapochezwa fainali ya kumtafuta bingwa mpya wa mkoa.

Katika mchezo huo wa fainali timu ya Veterans tayari wameshaingia fainali wakimsubiri atakaye chuana naye kati ya Magomeni United na Pangani City ambao wanacheza nusu fainali kutafuta tiketi ya kuingia hatua hiyo.

Kwa msimu huu wa ligi ya mkoa 2021/2022 inayotarajiwa kufikia tamati January 2 mwakani,Kampuni ya Rubi International inayofanya shughuli za madini mkoani Arusha imetoa zawadi ya vikombe kwa timu itakayochukuwa ubingwa.
Zawadi nyengine zitatolewa kwa kocha bora,mchezaji bora , mfungaji bora pamoja na timu yenye nidhamu ambayo itapewa hati ya kutambuliwa kushiriki ligi hiyo.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.