
RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Dk.
Rahma Salim Mahfoudh kuwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar.hafla
hiyo iliyofanyika leo 27-12-2021, katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Hussein Ali Mwinyi amewaapisha Wajumbe wapya wa Tume ya Mipango ya Zanzibar.
Hafla hiyo
imefanyika leo Ikulu Jijini Zanzibar ikiwa ni kikao cha kwanza cha Tume hiyo
katika Awamu ya Nane ya uongozi wa Rais Dk. Mwinyi ambapo Makamo wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman na
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah walishiriki ikiwa ni
Wajumbe kutokana na vyeo vyao.
Mara baada ya kiapo hicho, Rais Dk. Mwinyi alitumia
fursa hiyo kuwapongeza Wajumbe hao wapya aliowaapisha pamoja na wale wa zamani
wanaoendelea.
Katika pongezi
hizo, Rais Dk. Mwinyi alieleza matumaini yake makubwa kwa wajumbe hao wa Tume
ya Mipango ya Zanzibar katika kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Wajumbe
walioapishwa ni Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi
Mhandisi Zena Ahmed Said, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dk. Mwinyi Talib Haji,Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais Fedha na Mipango Mhe.Jamal Kassim Ali, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya
Makaazi Mhe.Riziki Pembe Juma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe.Mudrik Ramadhan Soraga.
Wengine ni Waziri
wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe.Omar Said Shaaban,Waziri wa Ujenzi,
Mawasiliano na Uchukuzi Mhe.Rahma Kassim Ali, Waziri wa Maji, Nishati na Madini Mhe.Suleiman Masoud Makame,Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Lela Muhamed Mussa,
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe.Abdalla Hussein Kombo pamoja na Dk. Rahma Salim Mahfoudh Kaimu Katibu
Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar.
Wajumbe hao
wapya walioapishwa hivi leo waliahidi kutekeleza majukumu yao kwa maslahi na
uchumi wa Zanzibar.
Nao wajumbe wa
zamani wa Tume hiyo ya Mipango ya Zanzibar Mohammed Faki Mohammed pamoja na
Profesa Semboja Haji Hatib walitoa
shukurani zao kwa Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi kwa kuendelea kuwaamini
kuwa Wajumbe wa Tume hiyo na kuahidi kwamba wataendelea kufanya kazi kwa ajili
ya maendeleo ya Zanzibar.
Imetayarishwa na Kitengo cha Habari.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Katibu wa Baraza la Mapinduzi
na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, kuwa Mjumbe mpya wa Tume ya
Mipango Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika leo 27-12-2021, katika ukumbi wa Ikulu Jijini
Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe.Dkt.
Mwinyi Talib Haji, kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika leo
27-12-2021, katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Fedha na Mipango Zanzibar.Mhe Jamal Kassim Ali,kuwa Mjumbe wa Tume ya
Mipango Zanzibar,hafla hiyo iliyofanyika leo 27-12-2021, katika ukumbi wa Ikulu Jijini
Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisaini hati ya Kiapo ya Waziri wa Ardhi,
Maendeleo na Makaazi Zanzibar Mhe.Riziki Pembe Juma, baada ya kumuapisha kuwa
Mjumbe wa Tume ya Mipango, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu
Jijini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Kazi Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mhe Mudrik Ramadhani Soraga, kuwa Mjumbe wa
Tume ya Mipango, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini
Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Waziri wa Biashara na Maendeleo
ya Viwanda Zanzibar Mhe Omar Said Shaban, kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango, hafla
hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano
Zanzibar Mhe. Rahma Kassim Ali, kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango, hafla hiyo
iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 27-12-2021 Jijini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Waziri wa Maji Nishati na Madini Zanzibar Mhe.Suleiman Masoud kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango, hafla
hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 27-12-2021 Jijini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Waziri wa Utalii na Mambo ya
Kale Zanzibar Mhe.lela Mohammed Mussa, kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango, hafla
hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 27-12-2021 Jijini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Waziri wa Uchumu wa Buluu na
Uvuvi Zanzibar Mhe. Abdalla Hussein Kombo,kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango, hafla
hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 27-12-2021 Jijini Zanzibar.
No comments:
Post a Comment