Habari za Punde

RC Ayoub awanasihi madereva kuzingatia sheria za Barabarani

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub M. Mahmoud amekutana na kufanya mazungumzo na madereva wa gari zinazobeba mchanga katika maeneo ya Donge Mchangani na kuwataka na kuwakumbusha madereva hao kuzingatia sheria za barabarani na kuwa na utamaduni wa kuendesha magari kwa mwendo mdogo ili kupunguza ajali ambazo zimekisiri katika Mkoa huo.

“Niwakumbushe madereva wetu wa magari ya mchanga, tumechoka na ajali katika Mkoa wetu, niwatake sasa kwenda kwa mwendo mdogo na mazingatio yote ya usalama barabarani” Mkuu wa Mkoa Kaskazini (U).
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub M. Mahmoud alipokuwa akizungumza na madereva wa gari zinazobeba mchanga katika maeneo ya Donge Mchangani 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.