Habari za Punde

V - Clean ya Turky kuimarisha usafi Zanzibar

Masheha mbalimbali wa Wilaya ya Mjini wakifuatilia uzinduzi wa mifuko maalum ya kuhifadhia taka pamoja na gari za kisasa za kubebea taka ngumu kwaajili ya kuimarisha usafi,hafla iliyofanyika viwanja vya kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge ,kwa udhamin wa V-CLEAN wakishirikiana na Baraza la Manispaa Zanzibar.
Muonekano wa gari za kusafirishia taka ngumu kwaaajili ya kuimarisha usafi zilizozinduliwa na Waziri wa Nchi (OR) Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ Mh.Masoud Ali Mohammed huko viwanja vya kumbu kumbu ya mapinduzi Kisonge, chini ya udhamin wa V-CLEAN wakishirikiana na Baraza la mji zanzibar.
Watendaji wa kampuni ya  Vigor wakifuatilia uzinduzi wa mifuko maalum ya kuhifadhia taka ,na gari za kisasa za kubebea taka ngumu kwa ajili ya kuimarisha usafi katika viwanja vya kumbukumbu ya mapinduzi Kisonge,kwa udhamin wa V-CLEAN wakishirikiana na Baraza la Manispaa Zanzibar.
Mwenyekiti wa  kampuni ya Vigor  Taufik Salum Turky akizunguma katika uzinduzi wa mifuko maalum ya kuhifadhia taka na gari za kisasa za kubebea taka ngumu kwa ajili ya kuimarisha usafi  ,hafla iliyofanyika viwanja vya kumbukumbu za mapinduzi Kisonge, chini ya udhamini wa wawekezaji  V-CLEAN wakishirikiana na Baraza la Manispaa Zanzibar.
Waziri *wa Nchi (OR) Tawala za Mikoa  na Idara maalum za SMZ Mh.Masoud Ali Mohammed  akikata utepe kuzindua gari za kisasa za kubebea taka ngumu kwaajili ya kuimarisha usafi ,hafla iliyofanyika viwanja vya kumbukumbu za Mapinduzi Kisonge.
Waziri wa Nchi (OR) Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ Mh.Masoud Ali Mohammed akizindua mifuko maalum ya kuhifadhia taka laini,taka za matumizi ya majumbani na taaka za mahotelini kwaajili ya kuimarisha usafi, hafla iliyoandaliwa na V-CLEAN wakishirikiana na Baraza
la Manispaahuko Viwanja vya kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge Zanzibar.
Waziri wa Nchi (OR) Tawala za Mikoa  na Idara maalum za SMZ Mh.Masoud Ali Mohammed  watatu kutoka kulia,Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrisa Kitwana,mwenyekiti kampuni ya vigor Taufik Turkey wakiwa na viongozi mbalimbali wa manispaaa ,  wakionyesha mifuko maalum ya kuhifadhia taka laini ,taka za matumizi ya nyumbani,na taka za hotelini ,mara baada ya uzinduzi WA mifuko hiyo huko viwanja vya kumbukumbu za mapinduzi Kisonge Zanzibar.

Waziri wa Nchi (OR) Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ Mhe.Masoud Ali Mohammed akiwa ndani ya moja ya gari alizozizinduwa kwajili ya kuimarisha usafi kupitia kampuni ya wawekezaji wa V-CLEAN ili kukagua zaidi gari hiyo,hafla iliyofanyika viwanja vya kumbukumbu za Mapinduzi Kisonge
*PICHA NA FAUZIOA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR.

Na Khadija Khamis -Maelezo 21/12/2021. 
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ.Mheshimiwa Masoud Ali Mohamed amewataka wananchi kuziunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha mji unakuwa safi. Kufanya hivyo kutaisaidia Zanzibar kuwa na haiba nzuri ambayo itaweka ustawi bora na kivutio kwa watalii wa ndani na nje ya nchi. 

 Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mifuko maalum ya kuhifadhia taka pamoja na gari za kisasa za kusafirishia zilizotolewa na Kampuni ya Vigor huko katika Uwanja wa Mapinduzi Square Kisonge . 

 Amesema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt,Husein Mwinyi ametoa rai yenye dhamira njema kuhakikisha mji unakuwa safi hivyo iko haja ya wananchi kushirikiana kwa pamoja kudumisha usafi katika maeneo yao. 

 Aidha alisema Kampuni ya V clean itashirikiana na Serikali kuondoa changamoto iliyopo ya kusambaa taka taka katika mji jambo ambalo linapoteza haiba na ustawi wa mji . 

 Alifahamisha suala la kujenga nchi sio la serikali pekee bali ni jukumu la wananchi wote hivyo iko haja ya mashirikiano ili kuhakikisha azma iliokusudi inafikiwa.

 Waziri Masoud alisema licha ya taka kuna uchafuzi wa mazingira ya kubandika matangazo mengi kiholela bila ya kufuata utaratibu kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa sheria. 

 Nae Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrisa Kitwana Mustafa alisema bado mji haujaridhisha hasa katika Mkoa wa Mjini Magharibi ambao ni jicho la Zanzibar hivyo sheria ndogo ndogo zitapitishwa kwa kutoa faini kwa wanaochafua mji . 

 Alisema ni vyema jamii kuimarisha mji kwa kupanda bustani mbali mbali katika maeneo yao ili kuengeza uzuri wa mji wa Zanzibar. 

 Nae Mkurugenzi wa Manispaa Mjini, Ali Khamis alisema Baraza la Manispaa kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji wa taka kumetokana na gharama kubwa ya uendeshaji, uchakavu na uwezo mdogo wa vifaa vya ukusanyaji wa taka pamoja na uchache wa rasilimali watu. 

 Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kampuni Vigor ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Mpendae, Taufik Salum Turkey amesema kampuni hiyo inamkakati wa kuzisarifu taka kwa lengo la kubuni miradi na kuzalisha viwanda vidogo vidogo vya vyakula vya kuku majongoo mbolea pamoja na karatasi jambo ambalo litasaidia kutoa fursa nyingi za ajira kwa vijana. 

 Akitoa wito kwa jamii alisema usafi ni jukumu la wote hivyo tushirikiane tuimarishe mji kwa pamoja na Kauli Mbio ya Uzinduzi huo ni Weka Mji Safi kwa Utalii bora Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.