Habari za Punde

Babu Duni ajitosa kugombea uenyekiti ACT

Makamu Mwenyekiti Mstaafu ya chama cha ACT wazalendo Juma Duni Haji akionyesha fomu aliyokabidhiwa Mjumbe wa kamati ya Uchaguzi ya chama hicho Muhene Said Rashid
 

Na Talib Ussi

Makamu Mwenyekiti Mstaafu ya chama cha ACT wazalendo Juma Duni Haji amechukuwa fomu ya kugombea uenyekiti wa Chama hicho huku akisema yupo tayari kukiongoza chama hicho ambacho kinakwenda kuchukua dola ya Tanzania katika uchaguzi ujao.

Hayo aliyasema wakati akichukua fomu ya kugombea nafasi hiyo ambayo alikabidhiwa kwake na Mjumbe wa kati ya uchaguzi Muhene Said Rashid katika ofisi za chama hicho iliyopo Mtaa wa Vuga Zanzibar.

“Nakwenda kuomba ridhaa ya kukiongoza chama ambacho ndicho kinachowapa Watanzanaia matumaini kwani ni chama chenye umoja mshikamano, ukweli na uadilifu.”alisema babu Duni.

Alisema ACT wazalendo ni chama kinachokuwa kwa kasi Tanzania na kufahamisha kuwa endepo atapata ridhaa ya wajumbe mkutano Mkuu Utakao Ufanyika January 29 Mwaka huu ataweza kusimamia vyema uendeshaji wa chama ikiwemo mfumo mpya wa kukusanya fedha kwa njia ya Mtandao ili chama kiweze kujiimarisha kifedha.

Duni amebainisha kuwa ataongoza chama hicho huku wananchi wakijua ni kwa nini wanapambana katika dhamira ya kutetea utu uzalendo na uadilifu kwa kile alichoeleza kuwa  chama chake ni imara kinachojenga hoja mbadala.

Alifahamisha  kuwa chini ya mwenyekiti yeye ataongoza chama kwa lengo la kuwatetea na kuwajaali watu na utu wao.

Akizungumzi suala tume za uchaguzi Duni alieleza kuwa haridhishwi na muundo wa tume zote mbili za Tanzania kwa maana  ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania NEC na ile ya Zanzibar ZEC.

“Tunataka tume   zote mbili   zibadilishwe na  mchakato wa katiba urudiwe sheria za uchaguzi zifanyiwe mapitio ili tupate tume huru “alisema babu Duni.

Amefahamisha kuwa ili nchi iendelee ni lazma kuwepo tume huru na haki na sheria za uchaguzi zifanyiuwe marekebisho kwa kuwepo chaguzi za huru na haki badala ya kila baada ya uchaguzi kuwepo matokeo ya vifo.

Mgombea huyo anayejuilikana Umaarufu wake wa babu Juma katika nafasi yake uwenyekiti kwa kushirikiana na wenzake atahakikisha kuna kuwepo mabadiliko makubwa katika chama hicho.

Akimkabidhi fomu ya kugombea Mjumbe wa kamati ya Uchaguzi ya chama hicho Muhene Said Rashid alimtaka mgombea huyo kurejesha fomu hiyo si zaidi ya tarehe 17 mwezi huu.

Nafasi ya Mwenyekiti katika Chama cha ACT Wazalendo imekuwa wazi tangu aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Maalim Seif Sharif Hamad kufariki Dunia hapo February 17 mwaka jana.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.