Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi awasili kisiwani Pemba leo kwa ziara ya kikazi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Chakechake Pemba na kusalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe Matar Zahor Masoud na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo, akiwa katika ziara ya Kikazi ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya Uzinduzi wa Miradi ya Maendeleo Kisiwani Pemba.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Serikali alipowasili Uwanja wa Ndege wa Chakechake Pemba akiwa katika ziara ya Kikazi ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar,kwa ajili ya  uzindua Miradi ya Maendeleo Kisiwani Pemba kesho 3-1-2022.(Picha na Ikulu)
 

STATE HOUSE ZANZIBAR

OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

PRESS RELEASE

Pemba                                                                                                02.01.2022---

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi  amewasili kisiwani Pemba leo kwa ziara ya kikazi ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za miaka 58 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Rais Dk. Mwinyi aliagwa na viongozi mbali mbali wakiongozwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah ambapo baada ya kuwasili kisiwani humo akiwa amefuatana na mkewe Mama Mariam Mwinyi alipokewa na viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa na Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Matar Zahor Masoud.

Akiwa kisiwani Pemba, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi hapo kesho (Januari 03.2022) mapema asubuhi anatarajiwa kushiriki katika ufunguzi wa Matembezi ya Vijana wa UVCCM Zanzibar huko Konde, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi baada ya shughuli hiyo anatarajiwa kuwasili Kinyasini Wete kwa ajili ya kuweka jiwe la Msingi Kiwanda cha kutengeneza Maji Safi Watercom (T) Ltd na baadae kuwahutubia wananchi.

Imetayarishwa na Kitengo cha Habari,

Ikulu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.