Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Ametoa Salamu za Pole kwa Jamaa na Marafiki Pamoja na Ndugu.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametoa salamu za pole kwa ndugu jamaa na marafiki pamoja na wadau wa habari wote kufuatia ajali ya gari iliyotokea Wilaya ya Busega, Mkoani Simiyu na kusababisha vifo vya watu wakiwemo waandishi wa habari.

Katika salamu hizo za rambirambi,  Rais Dk. Mwinyi alieleza kusikitishwa na vifo hivyo na kuwanasihi ndugu, jamaa na marafiki pamoja na wadau wote wa habari kuwa na subira na ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu cha misiba hiyo.

Rais Dk. Mwinyi amemuomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za Marehemu mahala pema peponi,  Amin.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi amemuomba MwenyeziMungu kuwaponya kwa haraka wale wote waliopata majeraha kutokana na ajali hiyo.

Imetayarishwa na Kitengo cha Habari,

Ikulu Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.