Habari za Punde

Maandalizi ya Uzinduzi wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Jumamisi Yakamilika

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Zanzibar Maishabora Foundation Bibi.Mwanaidi Mohamed Ali alipokuwa akizunagumza na Waandishi wa habari wa Vyombo mbali mbali kuhusu Uzinduzi wa Taasisi hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa tr 19 mwezi huu,ambapo mgeni rasmi atakuwa Mwenyekiti wake na Mke wa Rais wa Zanzibar Mhe.Mama Mariam Mwinyi.[Picha na Ikulu.] 17/02/2022. 
Waandishi wa habari walipata fursa ya kuuliza maswali wakati wa mkutano huo wa maadalizi ya uzinduzi wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

Na Mwashungi Tahir Maelezo      17/2/2022.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi anatarajia kuzindua Taasisi   ya Zanzibar Maisha Bora Foundation  kwa ajili ya kuwajali na kuwashajihisha makundi mbali mbali wakiwemo  wanawake, vijana na watoto ikiwa ni azma ya Serikali katika kuwakuza kiuchumi wananchi wake.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Wizara ya Utalii Kikwajuni  Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasis hiyo Mwanaidi Mohammed Ali  kwa niaba ya Mama Mwinyi amesema Taasisi hiyo itazinduliwa tarehe  19/2/2022 siku ya jumamosi katika Uwanja wa Mao zedong.

Amesema katika uzinduzi huo kutafanyika matembezi kuanzia Kiembesamaki Butros kupitia barabara ya Mazizini, Kilimani chini  , Miembeni, Michenzani hadi kumalizia Uwanja wa Mao ze dung na kutolewa huduma mbali mbali za uangalizi wa afya  kwa wananchi wote.

Aidha amefahamisha kuwa huduma zitakazotolewa hapo za afya ni  pamoja na  kupima sukari, kupima uzito, kuchangia damu, kufanyiwa uchunguzi wa macho, kupata chanjo ya UVIKO 19. Meno  na baadhi ya maradhi mengine ambazo huduma hizo zote zitatolewa bure.

Pia amesema matembezi hayo yatapofanyika wananchi wajitokeze kwa wingi na kwa wale watakaokuwa hawawezi kwenda sehemu zote wanaruhusiwa kukaa barabarani au hata kusubiria hapo kwenye kiwanja cha Mao zedong ni kumuunga mkono mama Mwinyi.

“Ikiwa mwananchi hawezi matembezi hayo kupita sehemu zote zilizotajwa anaweza kukaa barabarani au kuyangojea huko kwenye uwanja wa mao de zung ili na wao waweze kushiriki”, alisema mama Mwinyi.

Akizungumzia upimaji wa uviko 19 Mama Mariam amewasisitiza wananchi kupata chanjo kwani maradhi bado yapo hivyo endapo wananchi watajitokeza kupatiwa chanjo hiyo itasaidia kupunguza ukali wa maradhi hayo ambayo yameshamiri duniani kote.

Mama Mariam Mwinyi ameanzisha Taasisi hiyo kwa lengo la kuwaweka akinamama hasa wanaolima mwani   kuwaunga mkono na kuimarisha uchumi wa buluu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.