Habari za Punde

ZIARA YA WAJUMBE WA SEKRETARIETI YA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA MKOANI MARA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo (mwenye skafu) akiwa pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Ndugu Samweli Kiboye Nambatatu mara baada ya kupokelewa katika viwanja vya Nyatwali, Bunda mkoani Mara.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo (mwenye skafu) akiwa pamoja Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Ndugu Christina Mndeme wakiongozana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Ndugu Samweli Kiboye Nambatatu pamoja na Viongozi wengine wa CCM wa mkoa huo mara baada ya kupokelewa katika viwanja vya Nyatwali, Bunda mkoani Mara.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara Ndugu Ally Hapi (kulia) mara baada ya kupokelewa katika viwanja vya Nyatwali, Bunda mkoani Mara.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo (katikati) pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Ndugu Samweli Kiboye Nambatatu (kulia) wakiangalia daftari la orodha ya wanachama wa Shina namba 3, Buhemba, Wilayani Tarime, kushoto ni Mwenyekiti wa Shina hilo Ndugu Ibrahim Hamisi Werema.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akipandisha bendera kama ishara ya uzinduzi Shina namba 3, Buhemba, Wilayani Tarime, mkoa wa Mara.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo (katikati) pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Ndugu Samweli Kiboye Nambatatu (kulia) wakiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Kanali Michael Mtenjele mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Nyasaricho
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo  akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Nyasaricho kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime Kanali Michael Mtenjele (kushoto)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo  akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Nyasaricho, Tarime mkoani Mara(kushoto)
 (Picha na CCM Makao Makuu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.