Habari za Punde

Wadau wa Asasi za Kiraia Kisiwani Pemba Wapata Elimu Kuhusiana na Ukimwi.

AFISA kutoka Chama Cha Waandishi wa habari wanawake Tanzania, TAMWA Pemba Asha Mussa Omar, akichangia mada katika mkutano uliaondaliwa na Tume ya Ukimwi Zanzibar Ofisi ya Pemba na Kuwashirikisha wadau kutoka asasi za kiraia Pemba.
WADAU kutoka asasi za kiraia Pemba, wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa mada, uzingatiaji wa masuala ya Ukimwi katika sekta binafsi, mkutano uliofanyika katika ofisi za Tume ya Ukimwi Chake Chake Pemba.
MRATIB wa Tume ya Ukimwi Zanzibar Ofisi ya Pemba Ali Mbarouk Omar, akiwasilisha mada katika mkutano uliowashirikisha viongozi wa asasi za Kiraia, juu ya uzingatiaji wa masuala ya Ukimwi katika sekta binafsi, mkutano uliofanyika katika ofisi za ZAC Chake Chake Pemba.

MWAKILISHI kutoka jumuiya ya JUKAMKUM Pemba Dk.Ali Yussuf Ali, akichangia katika mada katika mkutano ulioandaliwa na Tume ya Ukimwi Zanzibar Ofisi ya Permba na kuwashirikisha wadau kutoka asasi za kirai Pemba.

(PICHA NA ABDI SULEIMAN)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.