.
Afisa Mikopo Mwandamizi wa Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Sophia Saidan akitoa huduma kwa wateja
mbalimbali waliotembelea Banda la HESLB leo
Jumapili (Machi 13, 2022) Mkoani Tanga wakati wa kampeni ya SIFURISHA
inayoendelea katika Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Tanga. Kampeni hiyo
inalenga kuhumasisha urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu kutoka kwa wanufaika.
Maafisa Mikopo wa HESLB wakitoa huduma
mbalimbali kwa wateja leo Jumapili Machi 13, 2022 Mkoani Tanga wakati wa
Kampeni ya SIFURISHA inayolenga kuhamasisha urejeshaji wa mikopo ya elimu ya
juu inayoendelea katika Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Tanga.
1. Meneja wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa
Elimu ya Juu (HESLB) Ofisi ya Arusha, PatricK Shoo akimkabidhi barua ya
kumaliza deni la Mkopo wa elimu ya juu TZS 11,345,845.20/- Milioni leo Jumapili
(Machi 13, 2022) Mkoani Tanga, Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Handeni,
Mhe. Yusuph Abdallah wakati wa kampeni ya SIFURisha inayoendelea katika Ofisi
ya Halmashauri ya Jiji la Tanga.
1.
Afisa Mikopo Mwandamizi wa HESLB, Sunday
Charles akimkabidhi barua ya kumaliza deni la mkopo wa elimu ya juu, TZS
9,736,900.90 Milioni, mtumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Mary Siphaelly leo
Jumapili (Machi 13, 2022) mara ya baada kulipa kiasi cha TZS 1,888,000/-
Milioni na kumaliza deni la mkopo huo
wakati wa kampeni ya SIFURISHA inayoendelea katika Ofisi za Halmashauri ya Jiji
la Tanga.
(PICHA NA HESLB)
No comments:
Post a Comment