Habari za Punde

HESLB Yazindua Mfumo wa Kidigitali wa Kurejesha Mikopo

  

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mfumo wa kidigitali unaomwezesha mwajiri kuwasilisha makato na orodha ya wanufaika-wafanyakazi wake kwa njia ya mtandao. Hafla hiyo ilifanyika jana Juni 10, 2022 Jijini Dodoma. Wengine pichani ni watendaji waandamizi wa HESLB na waajiri wa sekta binafsi mkoani Dodoma.


Na Eline Maronga. HESLB. Dodoma. 

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imezindua rasmi mfumo wa kidigitali unaomwezesha mwajiri kuwasilisha makato na orodha ya wanufaika-wafanyakazi wake kwa njia ya mtandao kutoka popote alipo.

 

Akizindua mfumo huo jijini Dodoma jana (Ijumaa, Juni 10, 2022), Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema mfumo huo ulianza kwa majaribio mwaka 2019/2020 na sasa umekamilika na hivyo kuwawezesha waajiri na wanufaika kurejesha mkopo kwa urahisi.

 

“Zamani ilikuwa mwajiri inabidi atoke ofisini kwake aje HESLB kufanya malipo lakini kwa sasa anaweza kuwasilisha orodha ya wanufaika-wafanyakzi wake na makato kutoka popote alipo kwa kutumia mfumo wetu huu ambao anajiunga kupitia tovuti yetu (www.heslb.go.tz),” amesema Mkurugenzi Mtendaji Abdul-Razaq Badru.

 

Kwa mujibu wa Badru, ambaye ameutangaza rasmi mfumo huo leo (Ijumaa, Juni 10, 2022) jijini Dodoma, mfumo huo pia unamwezesha mnufaika mmoja mmoja kupata taarifa za deni lake na utaratibu wa kurejesha kupitia tovuti ya HESLB.

 

“Kuanzia mwaka jana, imekusa ni rahisi sana, unaingia kwenye tovuti yetu, unabofya ‘rejesha mkopo’ au ‘repay loan’ na kufuata maelekezo ya kujisajili na utaendelea kupata taarifa ya deni lako palepale au hata kudai refund (makato yaliyozidi),” amesema Badru.

 

Akizungumzia uzoefu wake katika kutumia mfumo huo, mwakilishi wa Shule ya Msingi Young Jai iliyopo Dodoma, Bi. Young Mi Cha ameshauri HESLB iboreshe mfumo kuwawezesha waajiri kuwatambua waajiriwa wapya kama walinufaika na mikopo ya elimu ya juu.

 

“Kuna wakati waajiriwa wapya wanadanganya, hivyo pamoja na uzuri wa mfumo huu, ninashauri uboreshwe ili mwajiri aweze kutambua mwajiriwa mpya kama ni mnufaika wa HESLB au hapana bila kumuuliza au kuleta jina kwenu kwa uhakiki kwanza,” amesema Bi Young.   


HESLB ilianzishwa mwaka 2005 ikiwa na majukumu makuu mawili, kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji wanaojiunga na taasisi za elimu ya kukusanya mikopo iliyoiva kutoka kwa wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu tangu mwaka 1994/1995.


Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru (katikati) akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kidigitali unaomwezesha mwajiri kuwasilisha makato na orodha ya wanufaika-wafanyakazi wake kwa njia ya mtandao. Hafla hiyo ilifanyika jana Juni 10, 2022 Jijini Dodoma. Wengine pichani ni watendaji waandamizi wa HESLB na waajiri wa sekta binafsi mkoani Dodoma.

Mkurugenzi wa Urejeshaji na Urejeshwaji Mikopo wa HESLB George Mziray akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kidigitali unaomwezesha mwajiri kuwasilisha makato na orodha ya wanufaika-wafanyakazi wake kwa njia ya mtandao. Hafla hiyo ilifanyika jana Juni 10, 2022 Jijini Dodoma. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru na Meneja wa HESLB Ofisi ya Dodoma Octavia Seleman.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji waandamizi wa HESLB na waajiri wa sekta binafsi mkoani Dodoma.

(NA MPIGAPIGA WETU)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.