Habari za Punde

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Atoa Siku Tano kwa Wizara ya Kilimo Kukabidhi Pikipiki kwa Maafisa Ugani. *Asema ifikapo Jumapili Maafisa Ugani wawe wamekabidhiwa pikipiki zao

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua pikipiki zilizopo katika Ofisi za Wizara ya Kilimo jijini Dodoma,  Juni 8, 2022, ambazo zilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya Maafisa Ugani kote nchini. Waziri Mkuu ameiagiza Wizara  hiyo ihakikishe ifikapo Juni 12, 2022 (Jumapili) ziwe zimeshakabidhiwa kwa Maafisa Ugani. Kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Profesa Siza Tumbo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Profesa Siza Tumbo  (kushoto)  wakati alipokagua  pikipiki zilizopo katika Ofisi za Wizara ya hiyo Juni 8, 2022 jijini Dodoma, ambazo zilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya Maafisa Ugani kote nchini. Waziri Mkuu ameiagiza Wizara  hiyo kuhakikisha ifikapo Juni 12, 2022 (jumapili) ziwe zimeshakabidhiwa kwa Maafisa Ugani.

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku tano kuanzia leo Juni 8, 2022 hadi Juni 12, 2022      Wizara ya Kilimo iwe imeondoa pikipiki zote wizarani hapo na kuzikabidhi kwa wakurugenzi.               

“Hii haikubaliki, Wakurugenzi wote waandikiwe barua waje wazichukue, kama kuna ufungaji wa plate number utafanyika huko huko. Jumapili saa 10 jioni ziwe zimefika kwa wahusuka.”

 

Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Juni 8, 2022) alipokagua Ofisi za Wizara ya Kilimo zilizopo eneo la VETA, Dodoma na kukuta pikipiki zilizotolewa kwa ajili ya maafisa ugani zikiendelea kuwepo.

 

Aprili 4, 2022 Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alizindua ugawaji wa vitendea kazi vilivyoandaliwa na Wizara ya Kilimo kwa ajili ya Maafisa Ugani wote nchini. Vifaa ni pamoja na pikipiki.

 

Amesema tayari Mheshimiwa Rais Samia alishazikabidhi kwa ajili ya kupelekwa kwa maafisa ugani, hivyo kitendo cha pikipiki hizo kuendelea kubaki katika eneo hilo hakikubaliki.

 

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Profesa Siza Tumbo amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba wamepokea maelezo hayo na watayafanyia kazi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.